Na Mwandishi wetu
Viongozi wa Kitaifa wa Jumuia ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) wameanza ziara yao Manispaa ya Kigoma/Ujiji iliyopo Mkoani Kigoma leo October 26,2021 ikiwa ni ziara yao ya kwanza tangu kuchaguliwa kushika nyazifa hizo
Ziara hiyo imehusisha Mwenyekiti wa ALAT-Taifa Mhe. Murshid Ngeze akiwa na Katibu Mkuu Mtendaji wa ALAT-Taifa Ndugu. Elirehema Moses Kaaya kwa lengo la kutembelea miradi inayotekelezwa katika Manispaa hiyo na ufuatiliaji wa Ukusanyaji na matumizi ya mapato ya ndani
Ziara hiyo imetanguliwa kwa viongozi hao wa Kitaifa kufanya kikao na Watumishi wa Manispaa hiyo huku wakiwataka watumishi hao kuendelea kufanya kazi kwa uaminifu kwa lengo la kuleta maendeleo ya wananchi
Aidha Mwenyekiti huyo wa ALAT- Taifa ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kupeleka fedha za Kitanzania Million mia tisa sitini (Tsh 960,000,000/=) za ujenzi wa vyumba vya madarasa arobaini na nane (48) kwa Shule za Sekondari za Manispaa hiyo huku akiwataka wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo kama vile kuchangia fedha na nguvu kazi
Wakiwa katika Shule ya Sekondari Mlole wameendelea kuipongeza Serikali kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya maabara kwa shule za Sekondari na kukuza usomaji wa wanafunzi wa Masomo ya Sayansi mashuleni ambapo katika shule hiyo Serikali imetoa kiasi cha Fedha Million sitini (Tsh 60,000,000/=) ya ujenzi wa maabara ya Bailojia na Phizikia
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Athuman Msabila akiwasilisha taarifa kwa Viongozi wa ALAT-Taifa amesema kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 Manispaa ya Kigoma/Ujiji imepitishiwa jumla ya Tsh 31,949,472,000/= ikiwa Mishahara ni Kiasi cha Tsh 19,120,360,000/=, matumizi Mengineyo ni Tsh 800,815,000/=na Tsh 9,171,583,000/= kwa ajili ya miradi ya Maendeleo na Tsh 2,856,714,000/= ikiwa ni makusanyo ya Mapato ya ndani
Miradi mingine iliyotembelea ni pamoja na ujenzi wa madarasa matatu shule ya Msingi Mwasenga yakigharimu kiasi cha million sitini (Tsh 60,000,000/=), ukamilishaji wa Ujenzi wa jengo la Upasuaji na wodi ya wazazi katika kituo cha afya cha Gungu ukigharimu kiasi cha Fedha Million mia mbili sabini (Tsh 270,000,000/=, kutembelea kikundi cha wajasiliamali cha Mshikamano kilichopo eneo la Gungu kikjishughulika na utengenezaji na uuzaji wa fenicha ikiwa kimenufaika mkopo asilimia kumi (10%) kutoka katika mapato ya ndani kiasi cha fedha za Kitanzania Million kumi na mbili (Tsh 12,000,000/=)na kutembelea Soko la Mwanga
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa