Na Mwandishi Wetu
Waratibu elimu Kata na Walimu Wakuu wa Shule za Msingi tano (05) zenye kiwango cha mdondoko wa Wanafunzi (kuacha/kukatiza masomo) wameanza mafunzo ya siku mbili (02) yenye lengo la kudhibiti na kukabiliana na tatizo hilo katika Shule zao.
Mafunzo hayo yanafanyikia Shule ya Msingi Muungano yakitolewa na Wataalamu kutoka Ofisi ya udhibiti ubora Manispaa na kudhaminiwa na Mradi wa Shule bora.
Akizungumza katika Mafunzo hayo Mwezeshaji na mdhibiti ubora wa Shule Bi. Ester Lulakuze amesema mafunzo yalenga kuwawezesha Viongozi wa elimu ngazi ya Shule kutambua vikwazo na sababu za mdondoko na namna ya kukabiliana nao.
Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha kila Mwanafunzi anayeanza masomo anahitimu katika ngazi zote za kielimu.
Viongozi walioshiriki katika Mafunzo hayo ni kutoka Shule ya Msingi Kagera, Airport, Kikunku, Kichagachui, na Kiheba.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz #shulebora
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa