Na Mwandishi Wetu
Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Kigoma na Baraza la Madiwani Manispaa ya Kigoma/Ujiji leo September 13, 2021 zimejengewa uelewa juu ya kiwanda cha Mbolea kinachotarajiwa kujengwa Kata ya Kibirizi eneo la Katosho
kikao hicho cha uelewa kimefanyika chini ya Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Ester Alexander Mahawe katika Ukumbi wa Manispaa hiyo ambapo Shirika la Utunzaji Mazingira Ziwa Tanganyika (LATAWAMA) ndilo Mfadhiri wa Ujenzi wa kiwanda hicho
Mkurugenzi wa Shirika la Utunzaji Mazingira (LATAWAMA) Ndugu. Didier Cadelli amesema kiwanda hicho cha kuzalisha Mbolea kitasaidia kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao kwa wakulima waliopo Mkoani Kigoma, Mikoa jirani na Nchi jirani kama Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo
Amesema kiwanda hicho kitakachojengwa kitatumia malighafi za taka zinazooza zinazozalishwa majumbani na masokoni ambapo zaidi ya Tani mia moja na arobaini (Tonnes 140) za taka huzalishwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa siku na asilimia sitini (60%) ya taka hizo ni taka zinazooza
Meya wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Mhe. Baraka Lupoli amesema Manispaa ya Kigoma/Ujiji iko tayari kwa ajili ya ujenzi huo wa kiwanda kitakacholeta ajira kwa wakazi wa Manispaa hiyo na kuinua uchumi wa wakulima wa Mkoa wa Kigoma na Nje ya Mkoa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Athumani Msabila ametoa wito kwa wakazi wa Manispaa hiyo kuchagamukia fursa ya ukusanyaji taka huku akisema taka sio uchafu bali ni malighafi inayoweza kutengeneza kipato
Amewataka wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa Kata na Mitaa ambazo hazijaunda vikosi kazi vya usafi wananchi kuunda vikundi hivyo kwa ajili ya kukusanya taka na kuzipeleka katika maeneo yaliyotengwa na kujipatia kipato kutokana na shughuli hiyo
Ujenzi wa Kiwanda cha Mbolea Manispaa ya Kigoma/Ujiji utawanufaisha Asilimia sabini (70%) ya Wakazi wa Mkoa wa Kigoma ambao ni wakulima na tayari Wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji wamehamasishwa kuunda vikosi kazi vya usafi kwa kila mitaa ambapo wanakuwa wakipita katika makazi, taasisi za Serikali na zisizo za Serikali, na maeneo ambayo shughuli za kiuchumi hufanyika katika ukusanyaji wa taka, Mitaa thelathini na tatu (33) kati ya sitini na nane (68) zimeunda vikosi kazi vya usafi ambapo makusanyo ya fedha asilimia sitini (60%) hubaki kwa kikosi kazi huku asilimia (40%) huenda Ofisi ya Mkurugenzi kwa mjibu wa Sheria ndogo za Manispaa hiyo
Picha na video zaidi ingia katika maktaba ya picha kwa kubofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa