Na Mwandishi Wetu
Vyandarua zaidi ya laki moja na thelathini ( 133007) vinatarajiwa kugawiwa bure kwa Wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa lengo la kudhibiti na kupambana na ugonjwa wa malaria.
Yamebainishwa hayo Leo March 11, 2025 katika kikao cha Utoaji elimu kwa Wajumbe wa Kamati ya Usalama, Wakuu wa Idara na Wataalamu wa afya.
Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr. Rashid Chuachua amewataka Wananchi kutumia vyandarua watakavyogawiwa kikamilifu na kuepuka matumizi yasiyosahihi.
Akizungumza katika kikao hicho Mratibu wa Ugonjwa wa Malaria Manispaa ya Kigoma/Ujiji Dr. Shabani Magorwa amesema kiwango cha maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria katika Manispaa hiyo ni 8%.
Zoezi la ugawaji wa vyandarua linatarajia kufanyika kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Kigoma kwa kugawa kwa kila Kaya likienda sambamba na kumwagilia dawa za kuua wadudu na vimelea vya malaria.
#zeromalariainaanzanamimi
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa