Na Mwandishi Wetu
Wananchi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji wanatarajia kunufaika na vyandarua vyenye dawa 195,412 vitakavyogharimu fedha za Kitanzania zaidi ya Billion tatu (Tsh 3,908,240,000/=)kwa lengo la kudhibiti na kupambana na ugonjwa wa malaria.
Yamebainishwa Leo Mei 13, 2025 katika kikao cha kujadili taarifa za uandikishaji wa Kaya zitakazogawiwa vyandarua kilichohudhuriwa na Kamati ya usalama wa Wilaya ya Kigoma, Wataalamu kutoka wizara ya afya kupitia Kitengo cha kudhibiti Malaria(NMCP) na Bohari ya dawa (MSD) kilichofanyikia Kigoma Social Hall.
Akiwasilisha taarifa Mratibu wa malaria wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Dr. Shabani Magorwa amesema katika Kampeni ya uandikishaji na ugawaji wa Vyandarua umefanyika katika Kata zote 19 za Manispaa hiyo na jumla ya kaya 53,987 zimeandikishwa sawa 107.8%.
Amesema Maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria ni asilimia 6.6 huku akisema zoezi la unyunyiziaji wa viuadudu katika mazalia ya Mbu yaliyotambuliwa linatarajia kufanyika mara baada tu msimu wa masika kumalizika.
Akiongoza Kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr. Rashid Chuachua ameipongeza Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan kwa namna inavyohakikisha kila Mwananchi anakuwa na afya njema huku akisema atahakikisha vyandarua vinawanufaisha wananchi waliokusudiwa.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa