Na Mwandishi Wetu
Wadau mbalimbali wa elimu wametakiwa kujitokeza na kuweka mazingira bora ya ufundishaji na ujifunzaji kwa ujenzi wa Miundombinu ya Walimu na wanafunzi kwa lengo la kuinua na kuboresha viwango vya elimu katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Yamesemwa hayo na Mkuu wa idara ya Mipango na Uchumi Ndugu. Frednand Filimbi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Leo Februari 08, 2022 wakati akimuwakilisha katika zoezi la upokeaji wa zawadi kwa Wanafunzi waliofaulu kwa wastani wa juu kitaaluma katika Shule ya Msingi Gungu na Kikunku
Mkuu huyo wa idara amewapongeza wafadhiri wa Kigoma Elimu Foundation (KIEF) kwa kuendelea kutoa michango ya kielimu kila mwaka na utoaji wa motisha kwa Wanafunzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ambao wamekuwa wakifanya vizuri kitaaluma
Ameendelea kusema Mchango huo wa kielimu utainua viwango vya ufaulu kwa wanafunzi na kushika nafasi za juu katika mitihani ya kitaifa mashuleni na maendeleo ya Wanafunzi wenyewe
Aidha amewataka wadau wengine kujitoleza kwa kufadhiri miundombinu ya kielimu kama vile Vyumba vya madarasa, Vyoo, Nyumba za Walimu, ugawaji wa chakula na Uji mashuleni pamoja na taulo kwa wanafunzi wa kike
Awali akiwasilisha taarifa kwa Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa Kigoma Elimu Foundation (KIEF) Mkoani Kigoma Ndugu. Ismail Ally Kahenga amesema tangu Mwaka 2017 wamekuwa wakifadhili na kuweka mazingira mazuri ya Ufundishaji na Ujifunzaji kwa kujenga Miundombinu ya Umeme mashuleni, kulipia masomo ya ziada kwa wanafunzi, ugawaji wa sare za Shule na msaada wa ushauri wa kujiunga na shule na vyuo mbalimbali ambapo kwa Mwaka 2020 wanafunzi 180 walinufaika
Ameendelea kusema kwa Mwaka 2022 jumla ya wanafunzi 240 wa Shule za Msingi Rubuga, Kitongoni, Msingeni, Kichakachui, Kibirizi, Bangwe, Gungu, na Kikunku watanufaika kwa zawadi mbalimbali zenye thamani gharama ya Tsh. 3,600,000/= Kwa kugawiwa Daftari, kalamu, Rula, Mikebe na Fulana
Naye Afisa elimu Msingi Ndugu. Richard Mtauka amesema Manispaa ya Kigoma/Ujiji imeendelea kufanya vizuri kitaalamu katika Mitihani ya Kitaifa ambapo kwa miaka saba mfululizo katika Mtihani wa Kitaifa imeendelea kushikiria nafasi ya kwanza Kimkoa huku mwaka 2022 Wanafunzi waliofanya Mtihani Kitaifa wakiwa 5256 na wanafunzi 4644 wakifaulu sawa na asilimia 88 na kushika nafasi ya pili kimkoa
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kikunku amewashukuru wafadhiri hao wa Kigoma Elimu Foundation (KIEF) kwa zawadi zilizotolewa kwa Wanafunzi waliofaulu kitaaluma huku akisema imekuwa Motisha chanya katika kuhakikisha kila mwanafunzi anapenda kujifunza na kufaulu mitihani ya ndani na nje na matarajio ya wanafunzi yakiwa makubwa kutokana na zawadi zilizotolewa
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa