Na Mwandishi Wetu
Wadau mbalimbali wa elimu wametakiwa kujitokeza kusaidia Wanafunzi wenye ulemavu katika kuboresha ujifunzaji na kutimiza Ndoto zao.
Wito huo umetolewa na Mwakilishi wa Afisa elimu Msingi Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Cornel Kisinga wakati wa kukabidhi Viti Mwendo Viwili (02) kwa Walimu na Wazazi wa Kituo maalumu cha Shule ya Msingi Bushabani
Mdau wa Elimu aliyetoa vifaa hivyo ambaye pia ni Afisa Elimu Vielelezo na Takwimu Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Janeth Mollel amewataka Wadau wa elimu kuendelea kujitokeza katika kuwasaidia Wanafunzi wenye ulemavu kwa vifaa mbalimbali vya kujifunzia ikiwa ni pamoja na Chakula huku akisema wanatarajia kutoa bima za Afya kwa Wanafunzi hao.
Manispaa ya Kigoma/Ujiji ina Vituo nane (08) vya Elimu Maalumu vikiwa na Wanafunzi Mia nne hamsini na tatu (453) na Kituo maalumu cha Elimu Shule ya Msingi Bushabani kina Jumla ya Wanafunzi Arobaini na Saba (47), Wanafunzi wa Kiume wakiwa thelathini (30) na Wanafunzi wa kike wakiwa kumi na Saba (17).
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa