Na Mwandishi Wetu
Wadau wa Maendeleo Manispaa ya Kigoma/Ujiji wameahidi kuunga mkono juhudi za Serikali katika zoezi la utambuzì na uwekaji wa anwani za makazi kwa kuchangia fedha za kuwezesha zoezi hilo
Wameyasema hayo Leo March 03, 2022 katika kikao kilichoandaliwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kilichofanyika katika Ukumbi wa Joy in the Harvest kwa lengo la kuwajengea ulewa wa na kuwashirikisha katika zoezi hilo
Mgeni rasmi wa kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Ester Alexander Mahawe amewashukuru wadau hao kwa kuonesha na kuahidi kutoa fedha zitakazosaidia ununuzi wa nguzo, vibao vya mabati, na fedha za uratibu wa zoezi hilo
Amesema michango itakayotolewa atahakikisha inafanya kazi iliyokusudiwa ili kuhakikisha kila Mwananchi na mkazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji anakuwa na utambulisho wa mahali anapopatikana huku akimtaka Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kufikisha barua na fomu za mchanganuo wa bajeti kwa wadau hao wa Maendeleo ili kuchangia Kadri ya uwezo wao
Katika hotuba yake amewataka Wananchi kuhakikisha wanasimia zoezi hilo na kulinda miundombinu kama vile nguzo na vibao vitakavyosimikwa ili kutambulisha makazi na majina ya barabara
Aidha amesema kukamilika kwa zoezi hilo kutarahisisha Serikali kufikisha maendeleo kwa wananchi kwa urahisi kutokana na kujua miundombinu na huduma zinazopatikana kwa wananchi, upangaji wa bajeti, kuwezesha na kukuza Biashara Mtandaoni, upatikanaji kirahisi wa huduma za Jeshi la zima moto na Polisi
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi( CCM) Wilaya ya Kigoma Alhaji Yassin Mtalikwa amesema Chama hicho kinalidhishwa na utekelezaji wa ilani unafanywa na Viongozi wa Serikali ambapo pia amewataka wadau mbalimbali wa Maendeleo ikiwemo vyama vyote vya Siasa kuunga mkono zoezi hilo litakalolsaidia kufikisha maendeleo kirahisi kwa Wananchi
Nao baadhi ya wadau wa Maendeleo wakiwemo viongozi wa dini Paroko wa Kanisa la Roman katoliki Kigoma Mjini Padre Castus Rwegeshora na Mchungaji Eliudi Katona wameipongeza Serikali katika utekelezaji wa mpango wa anwani za Makazi na kusema wao kama taasisi za dini watahamasisha waumini wao kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo na kutoa fedha ili kutekeleza zoezi hilo
Naye mmoja kutoka katika Asasi za Kirai inayojishughulisha na msaada wa Kisheria Ndugu. Rufuano (kwa jina moja) amesema anaamini zoezi hilo litafanyika pasipo kizuizi chochote huku akiwaka wananchi kuendelea kuelimishwa kwa ajili ya kufanikisha suala hilo
Wadau wa Maendeleo waliohudhuria katika kikao hicho ni pamoja na viongozi kutoka Ofisi na taasisi za Umma, viongozi kutoka Mashirika ya Serikali na yasiyo ya Serikali, Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi, Vyama vya Siasa, Viongozi wa madhehebu ya Kidini, Watu Maarufu na Mashirika ya Kimataifa
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa