Afisa elimu taaluma sekondari Tabu Malima asema mtihani wa kidato cha sita na ualimu ulioanza jana may 7 umeanza katika hali ya uzuri, ameyasema hayo asubuhi ya leo akiwa ofisini kwake ambapo pia ametoa takwimu za walimu tarajali na wanafunzi walioanza mtihani huo wa kuhitimu taaluma pamoja na masomo ya wanafunzi hao
Afisa elimu taaluma huyo amesema idadi ya vituo vya mtihani katika manispaanya Kigoma/Ujiji vipo jumla ya saba(7) ambapo vituo vya watahiniwa wa shule(school candidate) vipo vitatu (3) vyenye jumla ya wanafunzi mia mbili tisini na nane(298) , vituo vya watahiniwa wa kujitegemea vipo vitatu(3) vyenye jumla ya wanafunzi mia moja ishirini na moja(121), na kituo kimoja(1) cha walimu tarajali chenye jumla ya watahiniwa kumi na tano(15) na kufanya jumla ya watahiniwa mia nne thelathini na nne(434)
Ameendelea kusema katika watahiniwa wote hakuna mlemavu aliyopo katika watahiniwa na kusema mtihani ulianza vizuri hapo jana na hakuna taarifa mbaya ambayo imeripotiwa katika vituo hivyo vyote vya mtihani kwa mitihahani ambayo imeshafanyika na ameendelea kusema wasimamizi wa mitihani hiyo wamepewa maadili ya kusimamia mitihani hiyo na kuwataka wasimamizi na wanafunzi kutojitokeza kwa hali ya udanganyifu wowote unaoweza kujitokeza.
Mtihani huo ulioanza jana kwa kidato cha sita may 7 ulianza kwa somo la general study kwa asubuhi na mchana yakafanyika masomo ya geography 1,French 1,na accountancy1, ambapo leo asubuhi yatafanyika masomo ya Kiswahili, basic applied mathemathics, advanced mathematics, na jion kufanyika englishi language, chemistry,na economics na mitihani hiyo inatarajia kukamilika may 18 mwaka huu kwa masomo ya phyiscs practical, computer science na Islamic knowledge kwa mikoa yote ya Tanzania bara na Zanzibar ambapo jumla ya watahiniwa wa shule(school candidate) 77,222 walianza mitihani hiyo nchini, watahiniwa wa kujitegemea 10,421 walianza mitihani na watahiniwa walimu tarajali 7,422 kwa ngazi ya cheti na stashahada nao pia walianza mitihani kwa kumitimu mafunzo ya taaluma ya ualimu.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa