Na Mwandishi Wetu
Wakandarasi wa ujenzi wanaotarajia kuomba kazi kupitia Mradi wa kuendeleza na kuboresha Miundombinu ya Miji Nchini Tanzania (TACTIC) leo March 24, 2023 wametembelea miradi inayotarajia kujengwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kupitia mradi huo
Wakandarasi hao wametembelea miradi inayotarajia kujengwa katika kipindi cha awamu ya Kwanza kwa lengo la kuitambua na kuona uhalisia katika kipindi cha utekelezaji kabla ya kuomba zabuni (Pre bid visting)
Barabara zilizotembelea na zinazotarajiwa kujengwa ni barabara ya Wafipa -Kagera yenye urefu wa Km 2.43 ikiwemo Ujenzi wa daraja la Mto Luiche , na barabara ya Bangwe-Burega-Ujiji yenye urefu wa Km 7.1
Miradi mingine iliyotembelewa na inayotarajiwa kujengwa ni Mitalo ya Maji ya Bangwe, Burega, Rutale, Mlole, Bushabani, Mji Mwema na Mtalo wa maji wa Katonyaga
Aidha miradi mingine inayotarajia kujengwa katika Mradi ya kuendeleza na kuboresha Miundombinu ya Miji Nchini Tanzania ( TACTIC) katika awamu ya Kwanza na ya pili ni pamoja na Ujenzi wa Kisasa soko la Mwanga, Ujenzi wa Kisasa wa Soko la mazao ya Uvuvi Katonga, na Ujenzi wa barabara ya Old Kasulu yenye urefu wa Km 7
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa