Na Mwandishi wetu
Wakazi wa Kijiji cha Nyabigufa kilichopo Kata ya Mkongoro Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma wameipongeza Serikali kwa kuwajengea daraja chini ya Wafadhili katika Mto Nyabigufa kutokana na kukosekana kwa huduma za jamii kabla ya daraja hilo
Wakazi hao wameelezea furaha yao mara baada ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2021 zikiongozwa na Luteni Josephine Paul Mwambashi kufika katika daraja hilo kwa lengo la kuzindua mradi huo
Daraja hilo lililogharimu kiasi cha fedha Million Mia Moja kumi na sita laki sita (116,600,000/=) likiwa limejengwa chini ya ufadhili wa Taifa la Ubelgi chini ya Shirika la Enable huku kiasi cha Millioni kumi na nne laki nne (14,400,000/=) ikiwa ni Mchango wa Wananchi na kiasi cha fedha Million tisa laki sita (9,600,000/=) ikiwa ni fedha za usimamizi kutoka mfuko wa Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini(TARURA)
Baadhi ya Wananchi akiwemo Bi. Ntayakila na Mzee Hassani Hamisi wamesema awali hasa kipindi cha Mvua wananchi walikuwa wakishindwa kuvuka katika mto huo na kufanya wananchi kushindwa kufika katika maeneo mhimu kama huduma za jamii ambapo baadhi ya wanawake walipoteza maisha kwa kushindwa kufika katika zahanati kwa lengo la kujifungua na wengine wakipoteza watoto wao kwa kushindwa kujifungua kwa wakati
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa akitoa salamu za Mwenge kwa Wananchi wa Kijiji cha Nyabigufa ameipongeza Serikali kwa kutafuta wafadhili waliowezesha kujengwa kwa daraja hilo ambalo limekuwa mkombozi kwa wakazi wa eneo hilo na maeneo jirani huku akiitaka Tarura kuendelea kufatilia utunzaji ya daraja hilo
Mbio za Mwenge wa Uhuri leo zimekimbizwa Wilayani Kigoma zikitokea Wilayani Uvinza ambapo jumla ya miradi nane (08) imetembelea, kuzinduliwa na kuwekewa jiwe la Msingi huku Jengo lakujifungulia na Upasuaji kwa wanawake katika kituo cha Afya cha Gungu likishindwa kuwekewa jiwe la Msingi kutokana na kutilia shaka matumizi ya fedha na TAKUKURU ikiamuliwa kufuatilia ujenzi mradi huo
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Kikundi cha wanawake wajasiriamali Tupendane kinachojishughulisha na uchakataji mise Simbo, Daraja la Mto Nyabigufa, Mradi wa Maji Matyazo Kalinzi, Mradi wa Jengo la kujifungulia na upasuaji kituo cha Afya cha Gungu, kutembelea ujenzi wa Madarasa Shule ya Msingi Kigoma,kutembelea Mifumo ya Tehama Ofisi ya Mkurugenzi, na uzinduzi wa Madarasa Shule ya Msingi Mwasenga ikigharaimu kiasi cha fedha za Kitanzania Billioni Moja Million arobaini na sita laki tatu na kumi na tano mia tano kumi na tatu (Tsh 1,046,315,513)
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa