Na Mwandishi Wetu
Manispaa ya Kigoma/Ujiji imeendelea kuzalisha kupitia Mapato ya ndani na kugawa bure miche ya Michikichi ya Kisasa aina ya Tenera kwa Wakulima.
Mapema Leo Novemba 05, 2024 Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr. Rashid Chuachua amegawa miche ya Michikichi ya Kisasa Elfu tisa mia sita hamsini (9650) kwa Wakulima ishirini na nane (28).
Akigawa Michikichi hiyo Mkuu wa Wilaya amewataka Wakazi wa Wilaya hiyo kuendelea kuwekeza katika kilimo hicho kutokana na Serikali kuweka nguvu katika upatikanaji wa Miche bure ili kuinua kipato cha Wakulima.
Awali akitoa taarifa Afisa Kilimo Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Pascal Bahati amesema kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 hadi 2023/2023 Manispaa ya Kigoma/Ujiji imezalisha na kugawa kwa Wakulima miche ya Michikichi ya Kisasa zaidi ya laki tatu na elfu sitini (360,620) na kunufaika kwa Wakulima mia nne sabini na tano (475).
Aidha amesema Miche 5,500 imepandwa kando kando ya barabara za lami katika mitaa kumi (10).
Kwa taarifa zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa