Na mwandishi wetu
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dr. Philemoni Sengati amewataka wananchi na wakulima wa kanda ya Magharibi ya maonesho ya nane nane yanayojumuisha Mkoa wa Tabora na Kigoma kuchagua viongozi bora watakaofanya siasa za maendeleo na wala sio vurugu kwa kuhakikisha uchumi wa Watanzania na Taifa unaendelea kukua
Ameyasema hayo leo Agusti 5, katika viwanja vya Fatuma Mwasa alipokuwa akizindua maonesho ya nane nane katika kanda ya magharibi kwa kuwataka wakulima na wananchi wote kufanya uchaguzi sahihi wa kiongozi aliye bora katika kuwatumikia wananchi kwa kuhakikisha wanampima kwa kumsikiliza sera za maendeleo na sio siasa za kuleta vurugu ndani ya Jamii za Watanzania
Mkuu wa Mkoa huyo amesema Kauli Mbiu ya Maonesho ya nane nane kwa mwaka huu ndio umeleta taswira chanya kuwa ili kuwaeza kuleta maendeleo katika sekta ya Kilimo, Mifugo, na Uvuvi ni lazima wananchi wafanye uchaguzi sahihi wa viongozi watakaowatumikia wananchi ili wasimamie maslahi ya wakulima hao na wanaojali maisha ya wanyonge walio wengi
Aidha mkuu huyo wa Mkoa amesema serikali ya awamu ya tano imejipambanua katika kuwatumikia wananchi wote hususani kuboresha mazingira ya wakulima, wavuvi, na wafugaji huku kwa kanda ya Magharibi Mkoa wa Kigoma 2019/2020 ukipata lita 600 kwa ajili ya dawa ya Josho kwa Mifugo na Mkoa wa Tabora ukipata lita 905 kwa mwaka , huku majosho ya kuogeshea N’gombe Mkoani Kigoma yakikarabatiwa nane(8) na Mkoa wa Tabora yakiboreshwa majosho siti ni na moja (61) kutokana na kuwa na maeneo mengi ya ufugaji katika Mkoa huo
Ameendelea kusema mikoa ya Kanda ya Magharibi inaongoza kwa kuwa na mifugo mingi ya Kienyeji huku akiwataka wakulima hao kuendelea kuboresha mifugo hiyo ili iweze kuleta tija katika uzalishaji kwa kuwatumia wataalamu waliopo ili kuweza kuhawilisha kwa kutumia mbegu Dume za kisasa huku mifugo na mimea ikilindwa dhidi ya Magonjwa wanaoshambulia kwa kufuata utaratibu wa kitaalamu pia
Aidha mkuu huyo wa Mkoa amesema kuanzia hivi sasa wakulima wa kanda ya Magharibi watakuwa wakifatwa na maafisa Ugani katika maeneo yao ya Ufugaji, kilimo na uvuvi kwa lengo kutatua changamoto zinazowakabiri na kumrahisishia mkulima na kumpunguzia adha ili kilimo hicho kikapate kuleta tija
Mkuu huyo wa Mkoa ameendelea kutaja mafanikio ya serikali ya awamu ya Tano kwa kupunguza migogoro baina ya wafugaji na wakulima zilizokuwa zikiendelea kwa kusema serikali ya awamu ya tano imeendelea kupunguza migogoro baina ya wakulima na wafugaji kutoingiliana katika utendaji kazi wao kwa kutenga maeneo maalumu ya kilimo na ufugaji
Akizungumza kabla ya Mkuu wa Mkoa huyo wa Tabora Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Kigoma Ndugu Rashidi mchata amewapongeza wakuu hao wa mikoa wapya kwa kuchaguliwa na Rais kwa lengo la kuwatumikia wananchi huku akisema Mkoa wa Kigoma kufikia mwakani wamepanga wawe wamehitimisha ujenzi wa majengo ya Maonesho ya nane nane hayo kwa Halmashauri zote kutokana na changamoto wanayomkumbana nayo ya kutokuwa na majengo ya mda na imara
Naye Mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo akizunguza katika mkutano huo Paul Tarimo amewapongeza kamati ya maandalizi kwa kuandaa maonesho hayo katika weredi Mkubwa kwa kuhakikisha miundombinu yote inayositahiri inakuwepo huku akiahidi kuwa kuna uwezekano mkubwa kitaifa Maonesho yajayo kufanyikia Kanda hiyo ya Magharibi huku akisema maonesho hayo Kitaifa kwa mwaka huu yatamalizika August 10 kutokana waziri wa Kilimo na Ushirika kuongeza siku mbili za maonesho
Ameendelea kusema serikali ya awamu ya Tano imesogeza huduma karibu na wakulima na wafugaji kwa kuhakikisha maafisa ugani wanapatikana katika kata mbalimbali ili kuweza kuwatukia wananchi kwa weredi na kuwasogezea wananchi huduma wanayoitaka huku akiwakumbusha wananchi wa kanda ya magharibi kuchangamkia zao la Korosho , Ufuta na Karanga kutokana na utafiti ulioonesha kuwa mazao hayo yanakubali zaidi katika ukanda huo
Naye Mwakilishi wa Wakulima wa Kanda ya Magharibi akisoma risala ameipongeza serikali ya awamu ya Tano kwa kuwa karibu kwa wataalamu ambao wameendelea kuwa mchango mkubwa katika shughuli zao za kila siku katika kulima mazao kama vile Tumbaku, Michikichi, Kahawa, na mihogo ambayo imekuwa mazao ya mda mrefu huku wakiomba kutafutiwa Technolojia itakayowasaidia kusonga mbele zaidi katika mazo ya kimkakati ya chakula na biashara
Mkuu wa Mkoa huyo kabla ya kuhutubia wananchi alitembelea mabanda mbalimbali kwa lengo la kuona kile wakulima, wafugaji na wakulima wamekuja kukionesha huku Mkuu huyo akiridhishwa na kufurahishwa na Banda la Manispaa ya Kigoma/Ujiji lililojengwa kwa uzuri na bidhaa walizokuja kuonesha kama ukuzaji wa zao la kimkakati la Mchikichi na uchakataji wa mafuta ya Mawese , techolojia ya ufugaji wa samaki wa kula na wamapambo pamoja na kilimo cha Bustani ya Chakula aidha amonesho hayo ya nane nane kwa mwaka huu yanaenda kwa Kauli mbinu kuwa “kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi , Chagua Viongozi Bora 2020.
Picha na video zaidi ingia www.kigomaujijimc.go.tz katika maktaba ya picha
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa