Na Mwandishi wetu
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Adengenye leo June 21, 2021 amewaapisha Wakuu wa Wilaya Wateule wa Wilaya za Mkoa huo huku akiwataka kujenga mahusiano mazuri na Wananchi na kusikiliza kero zao na kuzitatua kwa kufanya mikutano
Amewataka wakuu wa wilaya wote waliochaguliwa kuwatumikia wananchi kwa kusimamia miradi ya barabara, Maji, Umeme na miundombinu ya Afya na Elimu inayoendelea kujengwa katika Wilaya zao kwa kuhakikisha viwango na ubora wa miradi unazingatiwa
Ameendelea kuwataka Wakuu wa Wilaya hao kusimamia suala la ulinzi na usalama katika maeneo yao na kuhakikisha wanadhibiti upenyo wa wahamiaji haramu kuingia Nchini kupitia katika Wilaya za Mkoa huo kwa kuhakikisha vikao vya kamati za Ulinzi na usalama ngazi Mtaa na Kata vinafanyika na Wananchi wanashirikishwa
Aidha Mkuu huyo amewataka wakuu wa Wilaya kusimamia ukuaji wa uchumi kwa wananchi katika sekta ya kilimo kwa kuhakikisha pembejeo kwa wakulima zinapatikana na kuepuka kilimo cha mikono na kutenga maeneo ya uwekezaji kwa kila Halmashauri
Katibu tawala wa Mkoa wa Kigoma Ndugu. Rashidi Mchata akiongea katika uapisho huo amewapongeza wakuu wa wilaya kwa kuaminiwa na kuchaguliwa katika nafasi hiyo huku akiwataka kutoa ushirikiano kwa kuwatumikia wananchi wa mkoa huo
Wakuu wa Wilaya walioapishwa ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ester Mahawe, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu P 8608 Col.I.A Mwakisu, Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Col. E.M. Malasa, Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Hanafi Hassani Msabaha, Mkuu wa Wilaya ya Kibondo P 8310 Col. A.J. Magwaza na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Col. Michael Nyangalina
Uapisho huo umehudhuriwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ngazi ya Mkoa na Wilaya, Sekretarieti ya Mkoa,Wakuu wa wilaya wastaafu, Wakuu wa Taasisi za Serikali na zisizo za Serikali,Viongozi wa vyama vya Kisiasa, Viongozi wa dini, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Idara , Waandishi wa Habari na Wananchi
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa