Na Mwandishi Wetu
Mafunzo ya uandaaji na utengenezaji wa zana za kufundishia na kujifunzia kwa Walimu mahiri wa darasa la kwanza yalianza Jana Oktoba 08, 2025 katika Shule ya Msingi Kigoma.
Mafunzo hayo yanafanyika kwa Walimu wa Shule za Msingi za Manispaa ya Kigoma/Ujiji na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma chini ya Mradi wa Shule Bora.
Washiriki wa Mafunzo hayo Mwalimu Jetta Ndororo na Mwalimu Metus Steven wanasema mafunzo yanawajengea uwezo wa uandaaji wa zana za kufundishia na kujifunzia zinazorahisisha na kukuza viwango vya ujifunzaji wa Kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) kwa Wanafunzi wa darasa la Kwanza.
Shule Bora ni program ya elimu inayofadhiliwa na Serikali ya Uingereza chini ya Idara ya maendeleo ya Kimataifa (FCDO) ikilenga kuboresha elimu katika Shule za Serikali kwa ngazi ya elimu awali na msingi Nchini Tanzania.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa