Na Mwandishi Wetu
Wadau wa elimu Manispaa ya Kigoma/Ujiji Leo Januari 10, 2024 wamekutana na kujadiliana mikakati ya kuwarejesha Wanafunzi wenye umri wa Miaka 7-14 walioacha Shule kwa sababu mbalimbali.
Wadau waliokutana ni pamoja na Viongozi mbalimbali wakiwemo Madiwani, Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Watendaji Kata, Waratibu elimu Kata, na Viongozi wa dini.
Awali akitoa taarifa katika kikao hicho Afisa Elimu ya Watu Wazima Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Cornel Kisinga amesema Watoto wenye umri wa Miaka 7-14 wasio kuwa Shule ni Mia tisa sitini na tatu (963).
Amesema Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kuwarejesha wale waliokatiza masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo wale ambao hawakusajiliwa kabisa kuingia katika mfumo rasmi wa masomo.
Amesema Serikali imeendelea kushirikiana na Shirika la Kimataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kutoa vifaa vya Shule kama vile Daftari, kalamu, begi na taulo za kike.
Viongozi hao wamejadiliana na kuweka mkakati wa kuhakikisha wanaendelea kushirikiana na jamii ili watoto kurejea shuleni ikiwa ni pamoja na kupiga vita suala la utumikishaji wa Watoto.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa