Na Mwandishi Wetu
Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkurugenzi kwa Kushirikiana na Jeshi la Polisi wametoa mafunzo ya namna ya kukabiliana na kutokomeza Vitendo vya Ukatili wa mitandaoni kwa Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na Utangazaji (Ujiji Broadcasting Academy) kilichopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Akifungua mafunzo hayo Mratibu wa Dawati la Jinsia Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Aida Nzoa amesema mafunzo hayo yanalenga kuongeza uelewa na kuunganisha nguvu katika kutokomeza vitendo vya ukatili ndani ya jamii.
Amesema elimu hiyo inatolewa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yanayofanyika Novemba 25 hadi Desemba 10 Kila Mwaka.
Afisa Maendeleo ya Jamii Bi. Bernadetha Ntembeje amewataka Wanafunzi wa chuo hicho kupinga vitendo vya ukatili mitandaoni unaofanyika kupitia vifaa vya kidigitali kama vile Simu ya mkononi, Kompyuta, Saa janja, na Runinga.
Amewataka kutumia vifaa hivyo katika ujifunzaji wa masomo ya kitaaluma, na kutumia vifaa hivyo katika kuielimisha Jamii kupinga vitendo hivyo ambavyo vimekuwa vikiathiri hasa kundi la Wanawake na Watoto.
Amesema ukatili wa mitandao umekuwa ukisababisha madhara ya udharirishaji wa Kingono, Wasiwasi, na Vifo.
Kauli mbiu ya Mwaka huu " Tuungane kutokomeza Ukatili wa Kijinsia Mtandaoni".
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa