Na Mwandishi Wetu
Kamati za utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) Manispaa ya Kigoma/Ujiji Leo Julai 31, 2023 imetoa elimu ya kupinga vitendo vya Ukatili kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwananchi iliyopo katika Manispaa hiyo
Kamati hiyo imetoa mafunzo hayo yakifadhiliwa na Shirika la International Rescue Committee (IRC) linalojishughulisha na upingaji Ukatili kwa Wanawake na Watoto
Akitoa elimu katika Mkutano huo Mkuu wa dawati la jinsia na Watoto Mkoani Kigoma Inspecta Maiko Mjema amewataka Wanafunzi kutoa taarifa kwa Walimu pale wanapozuiliwa na Wazazi na Walezi kuhudhuria masomo na kutumikishwa shughuli za kiuchumi
Aidha amewataka Wanafunzi na Watoto kutoa ushirikiano kwa kutoa ushahidi kwa Jeshi la Polisi na Mahakama pale vitendo vya ukatili vinapofanyika ili kuchukua hatua za kisheria
Kwa upande wake Afisa Ustawi Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Siye Hara amewafafanulia Wanafunzi ukatili mbalimbali ambazo zinazoweza kutokea kama vile ukatili wa Kingono
Ameendelea kuwataka kutoa taarifa katika mamlaka husika ikiwemo Ofisi ya Mwalimu wa nidhamu au Mkuu wa Shule, Ofisi ya Mtendaji Kata au Mtaa, Jeshi la Polisi , Wazazi au Walezi pale vitendo hivyo vinapotokea
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa