Na Mwandishi Wetu
Wataalamu na Wadau wa elimu Manispaa ya Kigoma/Ujiji wamepata mafunzo ya kufanya tathimini ya mdondoko wa Wanafunzi kwa Shule jumuishi.
Mafunzo hayo yamefanyika chini ya mradi wa Shule bora yakihudhuriwa na Maafisa Elimu, Wadhibiti ubora wa Shule, Maafisa maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa jamii wakiongozwa na Mdhibiti ubora wa Shule Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu Amosi Nkomali.
Akizungumza katika Mafunzo hayo kiongozi huyo amesema Shule za Msingi tisa (09) kati ya Shule 47 zina changamoto ya mdondoko wa Wanafunzi (kuacha/kukatiza masomo) hali iliyosabibisha kufanya tathimini ili kujua viashiria, na kuitaka jamii kukabiliana na tatizo hilo.
Amesema timu hiyo ya Wataalamu itakutana na Walimu, Wazazi na Kamati za Shule na kuweka mikakati ya kukabiliana na viashiria vya mdondoko wa Wanafunzi.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa