Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Bi. Mwantum Mgonja amewataka Wananchi wa Manispaa hiyo kuendelea kutoa ushirikiano katika zoezi linaloendelea la kusasisha, kuhuisha na kukusanya taarifa mpya za Anwani za makazi.
Ameyasema hayo alipokuwa akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake mapema Leo March 19, 2024 kwa lengo la kuujulisha umma namna zoezi hilo linavyofanyika katika Kata na Mitaa yote ya Manispaa hiyo .
Aidha amewataka Wananchi kuendelea kutunza na kulinda miundombinu ya Anwani za Makazi inayowekwa kutambulisha Anwani kama vile vibao vya barabara na namba.
Naye Afisa Tehama kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na teknolojia ya habari Ndugu. Charles Semzaba amesema zoezi hilo linatekelezwa na Watendaji wa Kata na Mitaa kwa kusasisha taarifa katika mfumo wa Anwani (NaPA System) kutokana na mabadiliko ya taarifa mbalimbali.
Amesema zoezi hili la uhakiki, kusasisha na kukusanya taarifa mpya limeanza kwa Halmashauri kumi na tatu (13) Nchini na baadae kufanyika kwa Halmashauri zote.
Utambuzi na uwekaji wa Anwani za makazi Nchini ulifanyika na unafanyika kwa kutoa namba ya anwani (namba ya jengo, au kiwanja), majina ya barabara au kitongoji na postikodi.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz @wizarahmth @napennauye @ortamisemi
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa