Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma/Ujiji Dr.Rashid Chuachua Jana April 15, 2024 alifanya ziara ya kutembelea Kampuni na taasisi za uzalishaji wa miche ya Kisasa ya zao la michikichi.
Ziara hiyo aliifanya kwa kampuni za uzalishaji ya Ndugu Development Foundation (NDF), FELISA, Kikundi cha Yangu Macho, Kitalu cha Manispaa Katosho, na Taasisi ya utafiti wa Mbegu za Michikichi ya Kisasa (TARI) huku akipongeza namna Halmashauri inavyozalisha miche na kuigawa kwa Wananachi na Wakulima bure.
Katika ziara hiyo Afisa Kilimo Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Pascal Bahati alisema Manispaa ya Kigoma/Ujiji tayari imetoa kiasi cha Million Ishirini (Tsh 20,000,000/=) kwa taasisi ya Ndugu Development Foundation (NDF) kwa ajili ya uzalishaji wa miche ya Michikichi ya kisasa aina ya TENERA 13, 333 na kuendelea kuigawa kwa Wananchi bure, ambapo hadi sasa miche ya Michikichi ya Kisasa 375,120 imeshazalishwa na kuigawa kwa wakulima 517 ambapo jumla ya hekta 2,985 zimepandwa katika mashamba ndani na nje ya manispaa.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa