Na Mwandishi Wetu
Wakazi na Wananchi wa Kata ya Kagera Manispaa ya Kigoma/Ujiji wameipongeza na kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita namna ujenzi wa mradi wa Hospitali ya Manispaa hiyo unavyowanufaisha
Wameyasema hayo Leo March 30, 2023 Katika eneo la Ujenzi unaendelea wakati wakitekeleza shughuli za ujenzi
Wamesema Mradi umetoa ajira kwa Vijana na Wanawake jambo ambalo linaleta chachu ya maendeleo kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja na familia
Hamis Mussa Kavinwa na Bi. Mwasiti Jumanne ni Wakazi wa Kata ya Kagera ambapo wamesema kukamilika kwa ujenzi huo kutaendelea kuboresha upatikanaji wa huduma za matibabu karibu na Wananchi na Wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Aidha wamesema kujengwa kwa Mradi huo kumeongeza ajira kwa Wajasiriamali na wauzaji wa Vyakula, Mafundi, Vibarua pamoja na walinzi wanaoendelea kufanya kazi za kila siku
Mradi huo umeajiri zaidi Watu sitini na tano (65) kwa sasa wakiwemo Mafundi Ujenzi, Vibarua, Wanaofyatua tofali, Wachimbaji wa kokoto na mchanga
Manispaa ya Kigoma/Ujiji inatekeleza Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya katika Kata ya Kagera ambapo Serikali imeleta fedha Za Awali kiasi cha Million Mia tano (Tsh 500, 000, 000/=) na tayari ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) linaendelea likiwa hatua ya Msingi
Tayari zabuni ya ujenzi wa Maabara imetangazwa na itaanza kujengwa hivi karibuni, Na katika eneo hilo jumla ya Majengo ishirini na nane (28) yanatarajiwa kujengwa kadri Serikali itakavyokuwa ikitoa fedha ili kukamilisha ujenzi wa Hospitali hiyo
Kwa kipindi cha Miaka miwili Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dr. Samia Suluhu Hassan Serikali imefanikiwa kuboreshaji utoaji wa huduma za afya ya Msingi kwa kujenga na kukarabati Hospitali za Halmashauri 135 kwa gharama ya fedha za Kitanzania Billion 123.53/=
Zaidi endelea kufuatilia kupitia mitandao ya Kijamii na tovuti kupitia www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa