Na Mwandishi wetu
Wananchi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji jana Novemba 22, 2021 walipewa elimu ya kushiriki shughuli za maendeleo ikiwemo ushiriki wa uandaaji wa bajeti za Halmashauri kuanzia ngazi ya mtaa
Elimu hiyo ilitolewa na Mchumi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Mwajuma Ally alipokuwa katika kipindi cha #morningtrumpet kinachorushwa na Cicora radio 98.9 kila siku saa moja hadi saa nne asubuhi
Katika kipindi hicho Mchumi huyo alisema kila Mwaka Kuanzia Mwezi Agosti hadi Septemba Maafisa watendaji Kata na Mitaa huelekezwa kufanya mchakato wa maandalizi ya bajeti kwa kuainisha vipaumbele vya maendeleo na miradi ambayo hujadiliwa katika Mkutano Mkuu wa wananchi wa Kata na kuwasilishwa katika vikao vya Bàraza la Madiwani kuanzia mwezi January hadi Mwezi March na ya Taifa huidhinishwa na Bunge la Jamuhuri ya Muugano wa Tanzania Mwezi Aprili – hadi Juni kila mwaka
Aidha amesema mikutano hiyo ya wananchi ni Mhimu kwa sababu hujadili Kuwezesha utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya jamii, Kuwezesha mgawanyo mzuri wa rasilimali
na husaidia kusimamia matumizi ya fedha za umma na hivyo kupelekea uwajibikaji wa Serikali kwa wananchi
Winfrida Bwire (Mtangazaji wa Kipindi hicho)
Mchumi huyo alihitimisha kwa kusema kila Mwananchi ana nafasi ya kushiriki katika kuidhinisha bajeti, kwa kuhudhuria mikutano ya hadhara katika ngazi ya Mtaa na kata yake pia kwa kuhudhuria katika Mabaraza ya madiwani au Bunge la bajeti kama msikilizaji hivyo Wananchi wahakikishe wanatumia fursa hiyo
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa