Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr. Rashid Chuachua amezindua kuanza kwa ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Kasimbu iliyopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Uzinduzi huo umefanyika Leo Februari 26, 2025 ambapo Wananchi wa Kata hiyo wameshiriki katika uzinduzi huo kwa kufanya shughuli za Ujenzi.
Akihutubia Wananchi katika eneo hilo ameipongeza Halmashauri kwa namna ambavyo imekuwa ikitenga fedha za mapato ya ndani ili kusogeza huduma za Maendeleo karibu na Wananchi huku akiwataka kuendelea kujitokeza kushiriki Shughuli za maendeleo ikiwemo usafi wa kila Mwezi.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kigoma Ndugu. Kaduro amesema Chama hicho kitaendelea kuisimamia Serikali ili kutekeleza miradi ya kimaendeleo na kuwataka Wananchi kuendelea kuunga mkono na kuwa na imani na Chama hicho.
Awali akiwasilisha taarifa Mtendaji wa Kata ya Kasimbu Ndugu. Richard Magai amesema tayari wameshapokea kiasi cha Tsh 63, 676, 400/= kutoka mapato ya ndani ambapo Wananchi wameshachangia tripu nne (04) za Mawe na trip Sita (06) za Mchanga sawa na gharama ya laki Saba na Sabini (Tsh 770,000/=).
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa