Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Ester Alexander Mahawe Jana Novemba 1, 2021 aliwataka Viongozi wa Serikali na Kisiasa kuwashirikisha Wananchi katika ujenzi wa Miradi ya Maendeleo Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Aliyasema hayo katika kikao cha kuweka mikakati na usimamizi wa ujenzi wa Madarasa arobaini na nane(48) kwa shule za Sekondari kikihusisha Waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa idara na Vitengo, Watendaji kata, Watendaji Mitaa, Wenyeviti Mtaa, Wakuu wa Shule na Viongozi wa bodi za Shule kilichofanyikia ukumbi wa Manispaa hiyo
Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka viongozi hao kufanya mikutano ya Wananchi mara kwa mara kwa kuwajulisha miradi inayotekelezwa katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kushiriki shughuli za kujitolea katika kuendeleza miradi hiyo
Alisema "Waheshimiwa Madiwani, Watendaji kata na Wenyeviti wa Mitaa mna wajibu wa kutoa taarifa ya miradi yote inayotekelezwa na Serikali na wadau wengine wa maendeleo katika maeneo yenu ya utawala na wananchi kuwa na uelewa ikiwa ni pamoja na kuisimamia na mradi kuleta tija kwa jamii"
Aidha aliwataka Viongozi hao akiwemo Mkurugenzi na Wataalamu wake kutembelea Mara kwa Mara miradi hiyo katika kipindi chote cha ujenzi utakapokuwa ukiendelea kwa lengo la kusimamia ubora na thamani ya fedha kwa kila darasa
Awali Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Athumani Msabila akiwasilisha taarifa alisema Manispaa ya Kigoma/Ujiji imepokea kiasi cha fedha za Kitanzania Million Mia tisa tisini (960,000,000/=) kwa lengo la ujenzi wa vyumba vya madarasa arobaini na nane (48) ikiwa ni pamoja na kupambana athari zilizotokana na Uviko-19
Aliendelea kusema fedha hizo zinatarajia kuwanufaisha wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujij kwa kutoa ajira kwa makundi mbalimbali kama vile Mafundi Ujenzi, wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi, wachimbaji mawe, kokoto, Mchanga na Mama lishe watanufaika kutokana na kukua kwa mzunguko wa fedha
Afisa Mchunguzi mwandamizi wa Takukuru Bi. Reonida Mshema alizitaka kamati za ujenzi kuwa wakweli katika manunuzi wakizingatia Sheria ya kupinga Rushwa kazini kifungu cha 15 na Kifungu 28 ikiwa ni kosa kupokea Rushwa kwa lengo la kutoa kazi na ubadhilifu wa mali za Umma
Diwani wa Kata ya Kasingirima Mhe. Abdalah Kiembe alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha za ujenzi wa miundombinu ya elimu huku akisema Wapo tayari katika kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za ujenzi wa madarasa hayo na miundombinu mingine jambo ambalo baadhi wakazi wa Manispaa hiyo wamekuwa wakishiriki kwa kutoa mda na fedha(mali) zao
Picha na video zaidi unapatikana Maktaba ya Picha katika tovuti ya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa