Na mwandishi wetu.
Wanasiasa na wataalamu wa halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji leo march 11, wamepokea mfumo wa taarifa za kijiografia(GIS) kwa furaha huku wakisema utasaidia katika uendeshaji wa halmashauri.
Wameyasema hayo katika ukumbi wa Lake Tanganyika ambapo mafunzo yamefanyika ya kuwafundisha namna mfumo huo wa GIS utakavyofanya kazi, ambapo mafunzo hayo yametolewa na wataalamu kutoka TAMISEMI chini ya mradi wa uendelezaji na ukuzaji miji kimkakati(TSCP).
Katika semina hiyo iliyohudhuliwa na wadau mbalimbali wakiwemo wanasiasa kutoka katika vyama vyao ambapo wawakilishi wametoka katika chama ACT-Wazalendo, Chama Cha Mapinduz(CCM), na CHADEMA, Madiwani lakini pia viongozi wa Masoko yaliyopo katika halmashauri na watalamu kutoka ofsi ya Mkurugenzi wakiwemo na watendaji wa kata.
Akifungua semina hiyo Meya wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Mhe. Hussein Ruhava ameshukuru TAMISEMI kwa kuamua kuanza mafunzo hayo kutolewa katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji kati ya halmashauri 8 zinazonufaika na mradi huo wa uendelezaji na ukuzaji wa Miji kimkakati Tanzania(TSCP).
Ameendelea kusema halmashauri ina kila sababu ya kusimamia vyanzo vya mapato kupitia mfumo wa taarifa za kijiografia(GIS) kwa kuwa Manispaa inayejegwa na wakazi wa manispaa wenyewe , wanasiasa na wataalamu waliopo huku akiwataka wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji wapokee mfumo huo kwa mikono miwili kutokana na faida yake.
Naye kiongozi wa msafari wa wataalamu kutoka TAMISEMI na World Bank(WB) Eng. Nanai akiongea katika semina hiyo amesema imefika hatua sasa za halmashauri kuendeshwa kisasa kutokana na mfumo wa ukusanyaji taarifa za Kijiografia(GIS).
Ameendelea kusema halmashauri itatakiwa iwe na taarifa za walipa kodi wote kwani tayari mfumo uko tayari kufanya kazi huku akiwataka wanasiasa, wataalamu na viongozi wa masoko na wafanyabiashara kuwa na nia njema na kufikisha ujumbe kwa wananchi suala hilo.
Naye mtaalamu wa mfumo wa taarifa za kijiografia kutoka TAMISEMI Bi. Grace (kwa jina moja) amesema wamekuja kwa ajili ya kuwezesha halmashauri kutumia taarifa na namna zitakavyokuwa zikichakatwa kuingizwa katika mfumo.
Ameendelea kusema ni wajibu wa kila halmashauri kuajili wataalamu wa GIS kutokana na mfumo wa utambuzi wa taarifa za watu wote wakiwemo wakazi, wafanyabiashara na shughuli zinazofanyika katika kila eneo la halmashauri kwa kuzingatia mitaa pamoja na kata zote zilizopo.
Ameendelea kusema katika mfumo huo hauna madhara kwa wananchi bali unafaida katika upatikanaji wa taarifa za kijiografia uendeshaji na usimamizi wa halmashauri maeneo ya Masoko na utambuzi wa makazi lakini pia ikienda sambamba na kupunguza gharama za uendeshaji wa halmashauri.
Naye mmoja wafanyabiashara aliyehudhulia mafunzo hayo na Mwenyekiti wa wafanyabiashara soko la Mwanga amepongeza kwa mfumo huo na kusema utaleta ufanisi katika utendaji kazi mzuri wa halmashauri kuwafikia wananchi katika kutoa huduma mbalimbali huku akiahidi wafanyabiashara kupokea mfumo huo katika hali ya uzuri.
Nao baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakichangia mada katika semina hiyo diwani wa kata ya Kigoma mjini Mhe. Hussein Kariango na Mhe Kacheche wamepongeza TAMISEMI kwa mfumo ambao wamekuja nao kwani utaweza kukuza mapato ya halmashauri na kuondoa migogoro baina ya wafanyabiashara wa halmashauri hiyo.
Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji mchumi wa halmashauri hiyo Ndugu. Frednandi Filimbi ameishukuru serikali kwa kuja na mfumo ambao utakuwa ni mkombozi katika uendeshaji wa halmashuri na kusema halmashauri kupitia watendaji na wataalamu wameupokea kwa mikono miwili na kuwataka wanasiasa nao kutoa ushirikiano katika maeneo yao ya utawala.
PICHA ZAIDI INGIA KATIKA MAKTABA YA PICHA.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa