Na Mwandishi Wetu
Viongozi wa Vikundi vya huduma ndogo za kifedha kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) wametakiwa kuimarisha vikundi vyao ili kukidhi vigezo vya kukopeshwa mikopo ya 10% ya Wanawake, Vijana na watu wenye ukemavu inayotolewa na Halmashauri
Viongozi hao wametakiwa na Mratibu wa Mpango wa Kunusuru kaya Masikini (Tasaf) Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Izack Vyabandi Leo June 28, 2022 alipokuwa akiongea na Wenyeviti, Makatibu na Wahasibu wa vikundi hivyo katika Mafunzo ya kuhamasisha wanufaika wa Tasaf kuweka akiba na kukuza uchumi wa Kaya zao
Mratibu huyo amesema Wanachama wa vikundi hivyo elfu tano mia tatu na arobaini (5340) ambao ni wakazi wa Mitaa 49 kati ya 68 iliyopo wanatarajia kunufaika na mafunzo hayo kutoka kwa viongozi wao, Wanawake wakiwa Elfu nne mia tisa kumi na moja (4911) na Wanaume wakiwa mia nne ishirini na tisa (429)
Ameendelea kusema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha vikundi vinaendelea kujiimarisha kiuchumi na kuwa na uwezo wa kujikimu kimaisha ili familia kuendelea kupata mahitaji ya Msingi na kuwa na Miradi mbalimbali ya kiuchumi
Aidha amewataka viongozi hao ambao vikundi vyao havijaanza mpango wa kuweka akiba na kukopeshana kuanza ili kunufaika katika kuwekeza katika Miradi mbalimbali kwa kuzingatia katiba na Miongozo waliyojiwekea
Bi.Maimuna Ibrahimu ambaye ni Mwenyekiti wa Kikundi cha juhudi kilichopo Mtaa wa Masanga Kata ya Gungu Ndugu. Dezidel Kalisa ambaye ni katibu wa Kikundi cha Ilakoze kilichopo Mtaa wa Gezaulole na kata ya Gungu wamesema mafunzo waliyoyapata wataenda kutoa mafunzo na maelekezo kwa wanachama wengine na kufanya vikundi hivyo vinajiimarisha kiuchumi kutokana na ruzuku ambazo wamekuwa wakiendelea kuzipata mara kwa mara
Katika mafunzo hayo kwa viongozi wa vikundi hivyo mada mbalimbali zimewasilishwa zikiwemo umuhimu wa kikundi kuwa na katiba, Usimamizi wa mikopo, utunzaji wa kumbukumbu, usimamizi na utatuzi wa migogoro
Mwezi March na April, 2022 zaidi ya fedha za Kitanzania Tsh Million 500 ziliwanufaisha walengwa elfu kumi na moja mia tano thelathini na mbili (11532) ambapo zaidi ya Shilingi Milion 226 zilitolewa kwa Taslimu huku fedha zingine zikitolewa kwa njia ya Miamala ya simu na benki.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa