Na Mwandishi Wetu
Wasichana na Wanawake wenye Umri wa Miaka 14-29 Manispaa ya Kigoma/Ujiji wanatarajia kunufaika na mradi wa Wezesha Binti unaotarajia kuwanufaisha Wanafunzi, Wachakataji wa mazao ya michikichi, Wafugaji wa nyuki, na wakulima wa zao la Alzeti.
Mradi huo ambao umeanza unaotarajia kufanyika kwa kipindi cha miaka mitano (2023-2027) ukihusisha kuwainua Wasichana Walioko shuleni na Nje ya Shule kama vile Wajasiriamali ukifadhiliwa na Shirika la Enabel la Nchini Ubeligi.
Akitambulisha Mradi huo Jana May 25, 2024 katika Ukumbi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Mkurugenzi wa Mradi huo kutoka Shirika la Enabel Bi. Denise Lapoutre alisema mradi huo unatekelezwa Mkoani Kigoma katika Halmashauri tano (05) kwa gharama ya Euro Million 25 ukilenga kuwainua Wasichana na Wanawake.
Aidha alisema Shule za Sekondari zipatazo tano (05) Manispaa ya Kigoma/Ujiji zinatarajia kunufaika na mradi wa Wezesha Binti kwa kuwainua kitaaluma na Kujenga miundombinu kama bweni na miundombinu mingine.
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Salum Kali aliipongeza taasisi ya Enabel kwa mradi huo huku akisema Uongozi wa Wilaya utatoa ushirikiano ili kuhakikisha Wasichana na Wanawake wanafikia ndoto zao.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa