Timu ya wataalamu kutoka benki ya dunia, ofisi ya Rais TAMISEMI , na wataalamu kutoka jiji la Arusha jana July 16 iliwasili katika halmashauri ya manispaa ya kigoma/Ujiji kukagua miradi inayofadhiliwa na benki ya dunia (WB) chini ya mradi wa uendelezaji wa miji ya kimkakati Tanzania (TSCP).
Timu ya wataalamu iliwasili mapema asubuhi katika ofisi ya Mkurugenzi wa manispaa ya Kigoma/Ujiji na kufanya kikao ambapo taarifa ilisomwa namna miradi ya TSCP ilivyotekelezwa na namna inavyotekelezwa.
Akiwasilisha taarifa ya miradi Mhandisi wa manispaa hiyo Eng. Wilfred Shimba alisema miradi ilitekelezwa na inayoendelea kutekelezwa ni pamoja na ujenzi wa barabara, ujenzi wa mifereji inayopita katikati ya makazi ya watu, ujenzi wa dampo, zoezi la ukusanyaji wa taarifa za kijiografia (GIS), ujenzi wa mifereji wa maji taka ndani ya manispaa hiyo.
Aliendelea kusema barabara zinazojengwa ndani ya manispaa hiyo ni nane(8) zenye urefu wa km 11.97 ambazo ni barabara ya Kaaya-Simu, barabara ya Mwanga-Kitambwe-Mwembetogwa, barabara ya Wafipa-Kagera, barabara ya Kagashe, barabara ya Kakolwa, barabara ya Nazarethi ya Nazareth-Ujenzi, barabara ya kuingia hospitali ya Maweni na barabara ya Burega, huku akitaja mifereji iliyojengwa inayopita katika makazi ya watu ikiwa ni Km 2.35 ambapo ni mfereji wa Mlole na mfereji wa Katonyanga ambapo miradi hiyo inatekelezwa kwa fedha za kitanzania Billion 18,626,006,976.27/=
Aliendelea kutoa taarifa ya ujenzi wa mifereji ya mifumo ya maji taka ndani ya manispaa hiyo ambapo mradi huo unatarajiwa kutekelezwa ndani ya miaka ishirini kuanzia mwaka 2020-2040 ambapo shughuli zitakazotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa maeneo ya vyanzo vya maji kuepusha mmomonyoko wa ardhi, ukusanyaji maji taka na kutibu maji taka hayo jambo litakalonufaisha wakazi wa manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa kuepukana na mmonyoko wa ardhi kutokana na athari za mvua na kuharibu makazi.
Aliendelea kusema mradi huo kwa sasa Manispaa hiyo imeingia mkataba na kampuni ya M/s Cheil Engineering Co. Ltd. In with DOCH Limited ina yoandaa mpango na ramani za mabwawa na mfumo wa maji taka ambapo tayari kampuni hiyo imeanza kazi tangu may 2019, na kukamilika may 2020 kwa kiasi cha dola za kimarekani 719, 428.00.
Ameendelea kusema miradi mingine iliyotekelezwa ni ya ukusanyaji wa taarifa za kijiografia katika kata 4 zilizopo ndani ya manispaa ya kigoma/Ujiji huku kata 15 bado hazijafanyiwa kazi ambapo ofisi ya Rais TAMISEMI inalifanyia kazi katika kutekeleza shughuli hiyo.
Naye mwakilishi wa Benki ya dunia Eng. Nanai amepongeza ripoti iliyotolewa huku akisema mpango wa uendelezaji wa miji kimkakati Tanzania (TSCP) ifikapo may 2020 mradi huo utafungwa kutokana na mda wake kuisha ambapo ulianza mwaka 2010 huku akisisitiza miradi inayoendelea kutekelezwa halmashauri ihakikishe inamalizika kwa wakati.
Naye Eng. Jovin Biguye kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi akiwa katika miradi inayotekelezwa alisema zipo changamoto ambazo zinajitokeza katika miradi hiyo ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa alama za usalama barabarani katika maeneo yanayojengwa, na kukosekana kwa vivuko vya mda kwa wakazi katika barabara zinazojengwa jambo ambalo mhandisi na msimamizi wa mradi huo Eng. Basaya watarekebisha katika changamoto zilizojitokeza.
Naye mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Mwailwa Pangani aliwashukuru kwa kuja kutembelea miradi inayotekelezwa katika halmashauri hiyo huku akiahidi kupitia wakandarasi waliowaweka wataendelea kusimamia na kufatilia miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati na kuweza kuleta manufaa kwa wananchi na wakazi.
Picha zaidi ingia katika maktaba ya picha.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa