Na Mwandishi Wetu
Wataalamu kutoka Benki ya Dunia Wameridhishwa na utekelezaji wa ujenzi wa Miundombinu ya vyumba vya madarasa kupitia mradi wa BOOST na SEQUIP Manispaa ya Kigoma/Ujiji
wameyasema hayo katika ziara waliyoifanya Leo Septemba 20, 2023 Manispaa ya Kigoma/Ujiji wakiambatana na Wataalamu kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Wizara ya elimu
Katika ziara hiyo Mratibu wa mradi wa BOOST kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI Ndugu. Reuben Swilla amepongeza Wataalamu na Wananchi kwa namna ambavyo wameendelea kusimamia ujenzi wa miradi ambayo itaongeza ari ya Wanafunzi kujifunza
Katika ziara hiyo Wametembelea Mradi unaosimamiwa na Taasisi ya elimu ya Watu wazima wa kuboresha elimu ya Sekondari kwa njia mbadala katika Shule ya Sekondari Mwananchi , Ujenzi wa Shule mpya ya Kiheba kupitia mradi wa BOOST, na Ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa lengo la kuboresha Elimu YA Sekondari kwa njia Mbadala- Burega
Manispaa ya Kigoma/Ujiji inatekeleza Ujenzi wa miundombinu ya Ujenzi wa Shule za Msingi mpya, Vyumba vya madarasa kupitia mradi wa BOOST wenye thamani ya fedha zaidi ya billion moja (Tsh 1, 467, 200,000/=)
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa