Na Mwandishi Wetu
Wataalamu wa Halmashauri na Mikoa ya Kigoma na Kagera wameahidi kutekeleza mradi wa BOOST kikamilifu Ili kuleta ufanisi na matokeo yaliyokusudiwa
Wameyasema hayo Mapema Jana Desemba 23, 2022 katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Kasulu wakati wa kufunga mafunzo ya siku mbili (02) yaliyokuwa na lengo la kuzijengea timu za utekelezaji wa mradi huo wa BOOST
Akizungumza katika katika mafunzo hayo kwa niaba ya Wahandisi wengine Mhandisi wa Ujenzi Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Elias Shirima alisema katika Mradi wa BOOST ambao utahusisha Ujenzi wa Miundombinu ya Madarasa watahakikisha wanasimamia kikamilifu katika kutoa Ushauri wa Kitaalamu na Kiutendaji
Naye Afisa Mipango, Uchumi na Mipango kutoka Halmashauri ya Biharamuro Mkoani Kagera Ndugu. Jasphone issanzu Mkurugu alisema Halmashauri zipo tayari katika kupanga bajeti za utekelezaji kikamilifu kwa kushirikiana na idara mbalimbali na kuhusisha mapato ya Ndani na ushirikishaji wa Jamii
Awali akihutubia washiriki hao kabla ya kufunga mafunzo hayo Katibu Tawala Msaidizi idara ya elimu Mkoa wa Kigoma Bi. Paulina NdigezĂ aliwataka Wataalamu hao kutekeleza kikamilifu afua mbalimbali zilizofundishwa
Mradi wa BOOST unatarajiwa kutekelezwa kwa mda wa miaka mitano (05) kwa Mwaka 2021/2022 hadi Mwaka 2025/2026 kwa fedha za Kitanzania Trillion 1. 15 sawa na Dola za Kimarekani Million Mia tano (500)
Katika fedha hizo Dola za Kimarekani Million 480 zitatumika katika program ya lipa kulingana na matokeo na Dola za Kimarekani Million 20 ni gharama za utekelezaji wa uwekezaji wa miradi
Jumla ya vyumba vya Madarasa 12, 0000 vinatarajia kujengwa, ununuzi wa vifaa vya kisasa vya Tehama kwenye Shule zaidi ya mia nane (800) za Msingi na Vituo vya Walimu, na uandaaji wa vifaa vya kufundishia na Kujifunzia kwa elimu ya awali
Wataalamu Waliohudhuria mafunzo hayo ni pamoja na Maafisa elimu, Walimu wakuu, Waratibu elimu Kata, Wahandisi, Maafisa Maendeleo ya jamii, Maafisa Ustawi wa Jamii, Wahasibu, Maafisa mipango na Uchumi, Maafisa Manunuzi, Wadhibiti ubora wa elimu pamoja na Maafisa Mawasiliano Serikalini
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa