Na Mwandishi Wetu
Timu ya ubainishaji wa Wanafunzi wenye mahitaji maalumu ngazi ya Halmashauri Leo June 12, 2025 wameanza mafunzo ya siku mbili (02) kwa lengo la kuwezesha Walimu ngazi ya Shule kubainisha Wanafunzi hao.
Mafunzo hayo yanafanyika chini ya Mradi wa Shule bora unafadhiliwa na Serikali ya Uingereza Kupitia Mfuko wa UK aid kwa Walimu, Maafisa Elimu Kata, Afisa Maendeleo ya Jamii, Afisa Ustawi, Daktari na mdhibiti ubora wa Shule.
Wakibainisha Wanafunzi wenye mahitaji maalumu wamesema miongoni mwao ni pamoja na Yatima, Viziwi, Albino, wenye ulemavu wa viungo, Usonji, Changamoto za ujifunzaji, wenye Vipawa na vipaji.
Akifungua mafunzo hayo Kaimu Afisa elimu Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Cornel Kisinga ameitaka timu hiyo kuzingatia mafunzo ili kuwezesha ubainishaji ngazi ya Shule na kuwawezesha Walimu kuwatambua na kuboresha ufundishaji na ujifunzaji.
Miongoni mwa mada zilizowasilishwa na zitakazowasilishwa ni pamoja na Dhana ya elimu Jumuishi, Changamoto na utatuzi wake, Afua stahiki na ubainishaji wa Wanafunzi wenye mahitaji maalumu na uandaaji wa darasa Jumuishi.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa