Maafisa ustawi wa jamii wakishirikiana na jeshi la Polisi manispaa ya Kigoma/Ujiji jana February 14, wamewaunganisha watoto kumi na sita na familia zao baada ya msako wa usiku uliofanyika na jeshi la Polisi.
Jeshi la polisi lilifanya msako huo usiku February 13 siku ya Jumatano, mwaka huu baada ya kubaini uwepo wa watoto waishio mtaani, wanaodhurula ovyo na kutumia mda mwingi wa usiku wakiwa katika mabanda ya video na katika kamali za mashine za kichina maarufu kama Game.
watoto hao wamebanishwa kuwa na umri kati ya miaka 4 hadi miaka 15 kutoka katika maeneo ya Vamia, katubuka, mlole, uwanja wa Ndege, Ujiji na mwingine mmoja akibainishwa kutoka katika halmashuri ya Kigoma na kukabidhiwa kwa maafisa ustawi wa halmshauri hiyo.
Akieleza Afisa ustawi wa jamii wa manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Saada Amani chanzo cha watoto hao kukimbilia mtaani ameeleza kuwa baadhi ya watoto ni kuwa watukutu nyumbani kwao, makundi rika na umaskini uliopo katika baadhi ya familia licha ya baadhi ya wazazi kuwapa watoto uhuru mwingi wa kujiamulia wanavyotaka kama kufika majumbani mda wa usiku bila kuonywa na wazazi wao na hatimaye watoto hao kufanya makazi mtaani huko wanapokuwa.
Aliendelea kusema watoto hao pindi wanapokuwa mtaani hujipatia ajira tofauti tofauti na wengine kutumikishwa jambo ambalo ni kinyume na sheria za kumlinda mtoto na kutoa onyo kwa wale watu wanaofanya vitendo hivyo kuacha mara moja.
Naye Afisa wa Jeshi la Polisi dawati la jinsia na watoto Bi. Merry (kwa jina moja) alisema zoezi hilo la kuwasaka watoto waishio mtaani litaendelea na kuhakikisha wanatokomeza watoto hao kwa kuwaunganisha na wazazi wao huku wazazi hao wakichukuliwa hatua za kufunguliwa mashataka kwa kuwatelekeza watoto wao.
Nao baadhi ya wazazi waliweza kueleza sababu za watoto kukimbia majumbani , Mama Moses wa mtaa wa Mabatini Mwanga alisema mtoto wake anatabia ya kutoroka nyumbani kutokana na mtoto huyo kutopenda kwenda shule jambo linalompa wakati mgumu katika kumshughulikia mtoto huyo.
Naye Baba aliyekabidhiwa mtoto wake Ally miaka 13 amesema mtoto wake alitoweka nyumbani zaidi ya mwaka mmoja uliopita kutokana na makundi ya marafiki zake jambo ambalo limekuwa likimuumiza na amekuwa akimuona mara moja moja akiwa mtaani licha ya kutochukua hatua yeyote huku akisubili mtoto huyo akue akiwa mtaani na baadae kumwendeleza katika fani yeyote.
Katika nyumba ambapo wazazi na walezi wamekabidhiwa watoto maafisa hao wamewaasa kuwa watoto hao hawataweza kurudi mtaani kama amani na chakula vitakuwepo huku wakikwepa kusababisha migogoro ya familia, kufanya kazi kwa kuzalisha chakula na kukumbuka malezi bora yanayofaa baba na mama wakiwa pamoja.
Picha zaidi ingia katika maktaba ya Picha.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa