Watu nane wasafiri kutoka nchini Congo na Burundi wametengwa eneo maalumu Manispaa ya Kigoma/Ujiji baada ya kuwasili nchini Tanzania kupitia bandari ya Kibirizi iliyopo mkoani Kigoma
watu saba ni raia wa Tanzania wanaofanya Shughuli za kusafirisha watu kutoka Mkoani Kigoma kwenda Katika Nchi hizo na Raia mmoja kutoka Nchini Congo ambaye amesema alikuwa anakuja Nchini Tanzania kwa ajili ya matibabu
Watu hao wametengwa eneo maalumu kutokana na Agizo la serikali la kutaka wasafiri wote wanaotoka Nchi zenye viashiria vya Ugonjwa huo kupimwa afya zao kwa mda wa siku kumi na nne
Kaimu katibu Tawala wilaya Bi. Lucia Oswald Chinguku ameendelea kuwataka wakazi wa wilaya ya Kigoma kuendelea kuchukua tahadhari ya Ugonjwa huo kwa kuepuka mazoea ya kusalimiana, kukumbatiana na kuendelea kunawa mikono kila mara kwa kutumia maji yanayotiririka na sabuni ili kuweza kuua vimelea vya ugonjwa huo
Akiongea Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Dr. Shabaan Magorwa amesema tayari watu hao wamepimwa vipimo vya awali ambapo wameonekana hakuna mwenye dalili za Ugonjwa wa Corona
Kaimu Mganga Mkuu huyo ameendelea kusema licha ya afya zao kuonekana ni nzuri watatengwa eneo maalumu kwa mda wa siku 14 na wataendelea kupata vipimo kwa mda wa siku hizo kila siku asubuhi na jioni
Wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji tayari wameshapata elimu namna ya kujikinga na kuchukua tahadhari za Ugonjwa huo kwa njia ya Vyombo vya habari, elimu mashuleni, Makanisani, Msikitini na matangazo ya sauti katika Makazi ya Watu.
Chukua Tahadhari kuepuka ugonjwa wa Corona.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa