Na Mwandishi Wetu
Watumishi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Leo Novemba 14, 2024 wamepata mafunzo ya Siku moja (01) ya namna ya kujikinga na Magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Mafunzo hayo yametolewa na Wataalamu wa Idara ya afya kwa lengo la kuelimisha na kuepuka madhara yatokanayo na magonjwa hayo kama vile Vifo, athari za kiuchumi, na kupoteza nguvu kazi.
Awali akiwasilisha Mada Afisa lishe wa Manispaa hiyo Bi. Mastridia Dionis Gapi amesema Magonjwa yasiyo ya kuambukiza hayawezi kuambukizwa kutokana na kukosekana kwa vimelea vya ugonjwa.
Magonjwa hayo ni pamoja na kisukari, Magonjwa ya moyo, Shinikizo la juu la damu, Magonjwa ya figo, Magonjwa ya upumuaji, kutetemeka, na Kupoteza kumbukumbu.
Amesema Magonjwa Haya yanasabibishwa na Mtindo mbaya wa Maisha kama vile Ulaji, Unywaji, uvaaji, na vile unavyopenda kutazama huku akiwataka kuhakikisha wanafuata kanuni za afya za Ulaji kwa makundi yote ya vyakula pamoja na kufanya mazoezi.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa