Na mwandishi wetu
Kamati ya Afya Manispaa ya Kigoma/Ujiji imewataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao wenye umri wa miaka mitano(05) hadi kumi na nne(14) kupata tiba kinga kwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele inayotarajiwa kutolewa siku ya Ijumaa May 28,2021 katika shule za msingi
Kamati hiyo ilikutana siku ya Ijumaa May 21, 2021 katika ukumbi wa Manispaa hiyo ikiwa ni mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele na kwa Mkoa wa Kigoma ikiwa ni Magonjwa mawili (02) yaani Kichocho na Minyoo tumbo huku Kitaifa yakiwa ni magonjwa matano Matende na Mabusha, Kichocho,Minyoo tumbo,Usubi na Trakoma
Akifungua kikao hicho Mgeni Rasmi ambaye ni kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndugu. Frednand Filimbi aliwataka wazazi na walezi kujitokeza kwa wingi kuwapeleka na kuwasimamia watoto wao kupata tiba kinga ili kuondokana na athari zitokanazo na magonjwa hayo
Aliendelea kusema ili kuweza kukua kiuchumi na kuwa na watoto wenye uwezo darasani hata katika shughuli za kila siku ni lazima jamii izingatie afya yao na ya watoto wao kwani kupuzia kupata chanjo kutasababisha magonjwa hayo kudhorotesha kufanya kazi kwa jamii na kuingia katika umasikini
Akiwasilisha taarifa Mratibu wa Magonjwa yasiyopewa Kipaumbe Manispaa ya Kigoma/Ujiji Benjamini Yustus alisema ili kujikinga na magonjwa hayo ya Kichocho na Minyoo tumbo wananchi wanapaswa kuacha tabia ya kujisaidia choo ndogo na kubwa katika vyanzo vya maji ili kuepukana na magonjwa hayo na kuacha tabia ya kutumia maji yaliyotuama sehemu moja na kwa mda mrefu
Aliendelea kusema athari za magonjwa hayo ni pamoja kwa kudumaa kwa ukuaji wa mtoto, kujisaidia kwa choo na ndogo na kubwa yenye damu, kuvimba kwa ini na bandama hali ambayo kama mtoto asipopewa kinga tiba mapema huathiri suala la ujifunzaji darasani
Mganga mkuu wa Manispaa hiyo Dr. Sebastiani Siwale alisema idara ya afya imejipanga kutoa dawa kinga Albendazol na Praziquantel kwa watoto elfu hamsini na mia mbili ishirini na tano (50,225) huku akiwataka wazazi kuwaruhusu watoto wao kutokana na mwaka 2018 walitoa dawa kwa watoto elfu arobaini na tatu na sabini na tatu (43,073) sawa na asilimia themanini na nane (88%) wakati walengwa walikuwa elfu arobini na nane mia tisa thelathini na sita (48,936)
Aliwahakikishia wazazi na walezi dawa hizo hazina madhara yeyote licha ya kuwa maudhi madogo madogo kama vile kichefu chefu, kutapika,tumbo kuuma na kutokana na maudhi hayo mtoto atapaswa kunywa maji ya kutosha licha ya uwepo wa wataalamu wa huduma ya kwanza kwa shule zote za Msingi zilizoandaliwa
Naye Afisa elimu Afya na Mazingira Bi. Bukeye Gunaguje alisema tayari walimu wamepewa mafunzo ya kusimamia watoto katika siku hiyo ya utumiaji dawa, na kwa shule za msingi wanafunzi wote watatakiwa kula chakula kabla ya kumeza dawa hizo ili kuepukana na maudhi madogo madogo
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa