Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Ndugu. Thobias Adengenye amewataka Wazazi wa Mkoa huo kutoa ushirikiano kwa Walimu wa Msingi na Sekondari katika kutokomeza utoro Shuleni
Ameyasema hayo leo Octoba 10, 2022 katika kikao kazi cha wadau wa elimu kilichofanyikia katika ukumbi wa jengo la NNSF uliopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa lengo la uzinduzi wa miongozo ya kielimu
Katika kikao kazi hicho Mkuu wa Mkoa amesema wazazi wana fursa kubwa katika kuhakikisha Wanafunzi (watoto) wanapata elimu kwa kuwahimiza kuhudhuria masomo na kufuatilia taaluma na ufaulu wao wawapo Shuleni
Aidha amewataka Maafisa elimu kufuatilia weredi wa ufundishaji wa Walimu ili kuepukana na baadhi yao kuwa watoro wa vipindi na kutohudhuria kazini
Akizungumza katika kikao kazi hicho Waziri wa kazi, ajira na Vijana ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini Profesa Joyce Ndalichako amewataka Viongozi na wadau wa elimu kila mmoja kwa nafasi yake kusimamia miongozo hiyo ya elimu ili kuinua ufaulu na taaluma katika mkoa huo
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma. Benedict Mwalyambi amesema Mkoa wa Kigoma Umepokea fedha za Kitanzania zaidi ya Billion arobaini na sita (Tsh 46, 190, 000, 000/=) kwa lengo la utekelezaji wa miradi ya Maendeleo huku zaidi ya fedha za Kitanzania Billion saba ( Tsh 7, 160, 000,000/=) ikipokelewa kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa kwa Shule za Sekondari
Awali akiwasilisha taarifa Katibu Msaidizi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Wilaya ya Kigoma Ndugu. Obadia Makoko amesema katika uboreshaji wa elimu mkoani Kigoma ujenzi wa miundombinu umeleta tija ya mahudhurio kwa wanafunzi huku akiitaka Serikali kuendelea kuboresha Motisha kwa Walimu waliopo kazini, na kuboresha suala la Usimamizi na ufautiliaji katika masuala ya elimu kwa kuzingatia mwongozo iliyozinduliwa
Naye mwenyekiti wa Walimu Wakuu Mkoa wa Kigoma Ndugu. Amando Amando ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuboresha Mazingira ya Elimu mkoani humo huku akiwataka Wasimamizi wa elimu kuzingatia mgawanyo Sawa wa Walimu katika maeneo ya utendaji kazi
Katika kikao hicho miongozo iliyozinduliwa ni pamoja na muongozo wa uteuzi wa Viongozi wa elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mikoa , mwongozo wa Changamoto katika uboreshaji wa elimu Msingi na Sekondari na nini kifanyike, na muongozo wa kitabu cha kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji katika kwa ngazi ya elimu msingi
Aidha kikao hicho kimehudhuriwa na Viongozi wa Sekratarieti ya Mkoa, Kamati za Ulinzi na Usalama Mkoa na Wilaya, Wakuu wa Wilaya, Waheshimiwa Wabunge , Wakurugenzi, Meya na Wenyeviti wa Halmashauri, Wakuu wa Idara na Vitengo, Maafisa elimu Kata, na Walimu Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa