Na Mwandishi Wetu
Wazee wa kata ya Kitongoni Manispaa ya Kigoma/Ujiji wameishukuru Serikali kwa kuwaandalia vitambulisho vya wazee vitakavyowasaidia kupata huduma mbalimbali katika taasisi za Umma ikiwemo matibabu ya bure
Yamesemwa hayo na Wazee hao wakati wakikabidhiwa vitambulisho hivyo na Diwani wa Kata ya hiyo Mhe. Himidi Omary katika Ofisi za Kata ya Kitongoni ambapo jumla ya Vitambulisho vya Wazee Mia moja ishirini na tisa (129) vimekabidhiwa kwa Wazee wa kata hiyo
Akiwakakabidhi vitambulisho hivyo amesema vitambulisho hivyo vilivyozalishwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa Mapato ya Ndani ni bora huku akizitaka taasisi mbalimbali kuwapa kipaumbele Wazee katika utoaji wa huduma
Naye Mwenyekiti wa Wazee Kata ya Kitongoni Mzee Ramadhani Juma ameipongeza Serikali kwa namna inavyoweka mikakati na kutekeleza namna ya kuwahudumia Wazee katika Maeneo mbalimbali waliyopo
Manispa ya Kigoma/Ujiji tayari imeshawatambua Wazee Elfu moja mia mbili themanini na tisa (1,289) kutoka katika Kata kumi na tisa (19) zilizopo katika Manispaa hiyo na Vitambulisho Mia tano sitini na nane (568 ) vya Kata sita (06) tayari vimezalishwa ikiwemo kata ya Kigoma, Bangwe, Mwanga Kusini, Machinjioni, Rubuga na Kata ya Kitongoni
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa