Wazee waishio katika halmashauri ya manispaa ya Kigoma/Ujiji ijumaa walikutana kwa lengo la kufanya uchaguzi wa viongozi wao.
Wazee hao walikutana katika ukumbi wa halmashuari ya Manispaa hiyo, huku uchaguzi huo ukisimamiwa na Kaimu Mkurugenzi wa halmshauri na Mkuu wa idara Elimu Sekondari Ndugu. Emmanuel Katemi.
Kaimu mkurugenzi aliwatangazia washiriki wote nafasi zinazotakiwa kupigiwa kura ikiwa ni pamoja na nafsi ya Mwenyekiti, Mwenyekiti Msaidizi, Katibu, Katibu Msaidizi, mhasibu, mwakilishi wanaume na nafasi ya mwakilishi wa wanawake.
Uchaguzi huo uliratibiwa na idara ya Afya chini ya Afisa ustawi Bi. Sada …….., akifungua kikao cha uchaguzi kaimu Mkurugenzi aliwataka wazee hao kupendekeza utaratibu upi utumike katika kuwapata viongozi kwa ngazi tofauti tofauti na utaratibu uliopendekezwa ikiwa ni kura kwa njia ya siri.
Naye kaimu Mkurugenzi huyo aliwatakia upigaji kura ulio mzuri, huku akiwaahidi kuwa haki itatendendaka kwa kila mhusika na uchaguzi huo utakuwa wa huru na haki.
Alieendelea kuwataka wazee kuwa makini katika kuchagua viongozi walio makini kwa kuwawakirisha vyema popote pale, na kuwataka kukubaliana na viongozi watakaotangazwa kutokana na kura zao.
Uchaguzi ulimalizika salama kwa nafasi ya mwenyekiti akitangazwa mzee Zuberi Kisongo, mwenyekiti msaidizi akiwa ni Tamasha shabani , katibu akiibuka mzee Kilozo Mussa Dunia, Mhasibu akiwa ni Hamisi Baruti, Nafasi ya Mwakilishi wa wanaume akitangazwa Mzee Kitita Juma Magogwa, na kwa nafasi ya mwakilishi wanawake akitangazwa Mzee Zalifa Husseini.
Akitoa pongezi Mwenyekiti aliyechaguliwa Mzee Zuberi Kisongo alishukuru kwa uchaguzi uliofanyika na wazee wote wa mji akiahidi kuwafanyia kazi na kuwawakilisha vyema katika mambo mbalimbali ya kiutendaji ndani na nje ya Manispaa.
Viongozi hao waliochaguliwa wataenda katika kikao cha kuchagua viongozi wa mkoa pindi watakapoitwa.
PICHA ZAIDI INGIA KATIKA MAKTABA YA PICHA
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa