Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(MB) Mhe Kasimu Majaliwa leo may 23, amewataka wakazi wa Mkoa wa Kigoma kuanza kupanda miche ya Kisasa ya michikichi kutokana na Nchi kutumia gharama kubwa kuagiza mafuta ya mawese yatokanayo na zao hilo kutoka mataifa mengine
Ameyasema baada ya kuwasili mkoani Kigoma katika ziara yake ya Kikazi mkoani hapo, Akiwa katika kitalu cha miche ya michikichi ya Kisasa Katosha kata ya Kibirizi Manispaa ya Kigoma/Ujiji ameipongeza halmashauri hiyo kwa jitihada za uandaaji wa kitalu hicho kwa lengo la kuwagawia wananchi michikichi hiyo bure pasipo gharama yeyote
Aidha Waziri Mkuu huyo ameendelea kusema kwa sasa Mawese yanaingia nchini kutoka Mataifa Mengine kwa fedha za kitanzania jumla ya Shilingi Billioni 445 hutumika kila mwaka kuagiza katika Nchi ya Malaysia na Nchini Burundi jambo ambalo wananchi kuanza kulima miche hiyo itaokoa kiwango hicho cha fedha
Waziri Mkuu huyo ameendelea kusema Kwa Mkoa wa Kigoma tayari miche ya kisasa millioni 1, 800,000 tayari imezalishwa na kusema tayari kituo cha utafiti cha zao hilo la michikichi kimeanzishwa katika mkoa huo eneo la Kihinga jambo litakalofanya kuinua kwa zao hilo na kuleta tija na kukuza uchumi wa Mwananchi mmoja mmoja, Mkoa na Taifa kwa ujumla
Waziri Mkuu huyo amehitimisha kwa kuwakumbusha wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na Ugonjwa wa Covid-19 kwa kuhakikisha kunawa maji safi yanayotiririka, kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima na kuvaa barakoa huku wakiendelea kufanya shughuli za uzalishaji mali
Akiwa katika kitalu hicho alipewa taarifa naKaimu mkuu wa idara ya kilimo, Ushirika na Umwagiliaji Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu Haruna Mtandanyi kuwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji ina lengo la kuzalisha miche ya michikichi ya kisasa Millioni moja (1,000,000) ambayo itagawiwa kwa wananchi bure ambapo kwa sasa mbegu elfu thelathini (30,000)zipo na miche zaidi ya elfu Kumi na saba tayari imepandikizwa katika kitalu sawa na asilimia 58.5% ya lengo la uzalishaji
Naye Meneja Sido Mkoa wa Kigoma amesema katika kuhakikisha zao la michikichi linakua na kukuza uchumi wa Mwananchi serikali imeleta mashine za kuchambua, kuchemsha na kukamua mawese na mafuta hayo kusafishwa kwa lengo la kupata mafuta yaliyo bora, ameendelea kusema tayari mashine hizo zimeanza kufungwa wilaya ya Buhigwe kijiji cha Janda ambapo mda si mrefu kijiji cha Kinazi na Bukuba vitafungwa mashine hizo ambapo matarajio ni kupata mafuta mengi zaidi kwa wakati mfupi
Naye Mmoja wa wakulima wa zao hilo katika bonde la mto Ruiche Mzee Mkala ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuja na mkakati wa kuinua zao hilo kibiashara na kuleta tija kwa Mkulima, huku akishukuru miche hiyo kugawiwa bure na kusema awali miche hiyo walikuwa wakinunua kwa kila mche Shilingi za Kitanzania 6000/- jambo ambalo lingeleta shida kwa wakulima katika kubadili na kuondoa miche ya zamani katika mashamba yao
Waziri Mkuu yupo Mkoani Kigoma kwa ziara ya Siku moja kukagua uendelezaji wa zao la kimkakati mkoani hapo , baada ya kukagua kitalu cha michikichi eneo la Katosho kata ya Kibirizi kiongozi huyo anaendelea kukagua uendelezaji wa zao la michikichi Gereza la Kwitanga na kushiriki upandaji wa zao hilo na kumalizia kukagua uendelezaji wa zao hilo katika Kikosi cha Jeshi 821 Bulombora
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa