Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr. Rashid Chuachua amewataka Wenyeviti na Wajumbe wa Serikali za Mitaa waliochaguliwa kuwatatua Changamoto zinazowakabili Wananchi katika Maeneo yao.
Ameyasema hayo Leo Novemba 29, 2024 alipokuwa akihutubia Wenyeviti na Wajumbe wa Serikali za Mitaa waliochaguliwa katika Uchaguzi uliofanyika Siku ya Jumatano.
Amewataka kuwahudumia Wananchi ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha Wananchi kushiriki miradi ya maendeleo.
Aidha amewataka kuepuka na kupinga Vitendo vya rushwa katika kuwatumikia Wananchi ikiwa ni pamoja na kusoma Mapato na matumizi katika Mikutano ya hadhara.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa