Na Mwandishi Wetu
Wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Leo Desemba 3, 2022 wameendelea na maazimisho ya wiki ya Sherehe ya Miaka sitini na Moja (61) tangu Tanzania bara awali ikiitwa Tanganyika ilipojipatia Uhuru wake Desemba 9, 1961
Maadhimisho hayo yameendelea kwa Wananchi, Viongozi na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kasimbu iliyopo katika Manispaa hiyo kushiriki zoezi la upandaji wa zao la Mchikichi
Akizungumza katika tukio hilo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Idrisa Naumanga amewataka Wakazi wa Manispaa hiyo kuendelea na zoezi la upandaji wa miche ya kisasa ya zao hilo kutokana na uzalishaji wa mafuta ya Mawese kuwa mengi pamoja na malighafi zingine
Ameendelea kuwataka Wananchi kuendelea kuitunza na kuithamini miche hiyo iliyopandwa katika Shule ya Sekondari ikiwa ni alama ya kusherehekea miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania bara awali ikiitwa Tanganyika
Kaimu Mkurugenzi huyo ameiagiza idara ya Misitu na Mazingira kupandwa kwa miti mingine ya Matunda na kivuli katika Shule hiyo
Wakizungumza katika tukio hilo baadhi ya Wanafunzi wa Shule hiyo Ndugu. Ismail Samweli na Mashuma Swalehe wameipongeza Serikali kwa maadhimisho ya wiki ya Uhuru ya Miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania bara huku wakisema mazao waliyopanda itakuwa ukumbusho huku wakiahidi kuilinda na kuitunza
Katika Shule hiyo zaidi ya Miche hamsini (50) ya Miche ya Kisasa ya zao la michikichi imepandwa na Wananchi, Walimu, Wanafunzi na Viongozi mbalimbali wa Kata na Mitaa walihudhuria maadhimisho hayo
Tanzania bara awali ikiitwa Tanganyika kwa sasa inafahamika kwa jina la Tanzania kutokana na Muungano wake na Zanzibar mwaka 1964 na Kauli mbiu ya Mwaka huu ni " Miaka 61 ya Uhuru, Amani na Umoja ni nguzo ya Maendeleo yetu ".
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa