Na Mwandishi Wetu
Wananchi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Leo Desemba 2, 2022 wameanza kuazimisha wiki ya ya Sherehe ya Miaka sitini na Moja (61) tangu Tanzania bara awali ikiitwa Tanganyika ilipojipatia Uhuru wake kutoka kwa Ukoloni wa Uingereza Desemba 9, 1961
Wananchi hayo wamefanya maadhimisho hayo kwa kufanya Usafi katika Soko la Buzebazeba wakishirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma na Viongozi wa Manispaa kwa lengo la kuboresha na kukuza Usafi wa Soko hilo
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Ester Alexander Mahawe akiwahutubia Wananchi na Wafanyabiashara wa Soko hilo mara baada ya kukamilisha zoezi la usafi amewataka kujenga tabia ya Usafi kila siku hata katika makazi yao
Aidha amesema katika kuendelea kufanya Usafi kutawafanya kuepuka magonjwa ya mlipuko kama kipindu pindu hasa katika kipindi hiki cha mvua
Naye Meya wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Mhe. Baraka Naibuha Lupoli amewataka wanafanyabiashara hao kuendelea kuboresha Mazingira yao ya kazi kwa kufanya shughuli za Usafi ili kuwavutia wateja katika soko hilo
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndugu. Idrisa Naumanga amewataka wafanyabiashara kuzingatia Usalama wa afya za wauzaji na walaji huku akiwataka Wataalamu wa Afya na Mazingira kuendelea kufanya ukaguzi wa Usafi katika masoko mengine yaliyopo na Makazi katika kata na Mitaa mbalimbali
Miaka 61 baada ya Uhuru wa Tanzania bara awali ikiitwa Tanganyika na sasa inafahamika kwa jina la Tanzania kutokana na Muungano wake na Zanzibar mwaka 1964 na Kauli mbiu ya Mwaka huu ni " Miaka 61 ya Uhuru, Amani na Umoja ni nguzo ya Maendeleo yetu ".
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa