Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Salum Kalli Leo May 02, 2024 amezindua Wodi ya Wazazi katika kituo cha afya cha Buhanda kilichopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa lengo la kuanza kutumika.
Uzinduzi huo umefanyika ukihudhuriwa na Viongozi wa Serikali, Vyama vya siasa pamoja na Wananchi huku akikabidhi gari jipya la Wagonjwa (Ambulance).
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amekagua Mashine ya Utra Sound na kiti cha huduma ya Kinywa na Meno (Dental Chair) katika Kituo hicho cha afya.
Akizungumza katika tukio hilo Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Mwantum Mgonja ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa namna ambavyo imeendelea kuboresha huduma za afya kwa Wakazi wa Manispaa hiyo kwa kutumia zaidi ya fedha za Kitanzania Billion tatu (Tsh Billion 3.6/) kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba.
Amewahakikishia Wananchi kuendelea kutoa huduma za matibabu katika misingi ya uadilifu ikiwa ni pamoja na Manispaa hiyo kutenga fedha za Mapato ya ndani ili kuboresha Kituo hicho cha afya.
Zaidi endelea Kutembelea www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa