Na Mwandishi Wetu
Miradi ya Ujenzi Awamu ya kwanza yenye thamani ya fedha za Kitanzania zaidi ya Billion ishirini na tisa ( Tsh 29,813,388,456.50/=) kupitia Mradi wa kuendeleza na kuboresha Miundombinu ya Miji Nchini Tanzania ( TACTICS) Manispaa ya Kigoma/Ujiji inatarajia kuanza Novemba 01, 2023.
Yameelezwa hayo Leo Oktoba 23, 2023 katika kikao cha kukabidhi maeneo ya utekelezaji wa miradi (Sites) na kutambulisha mradi kwa Wadau mbalimbali kilichofanyikia Ukumbi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kikiongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bi. Mwantum Mgonja.
Katika kikao hicho imeelezwa miradi ya Ujenzi hiyo inatekelezwa na Wakandarasi kutoka Kampuni ya China CRJE EAST AFRICA, na Wahandisi washauri kutoka Ethiopian SABA Engineering na SELCA CONSULT TANZANIA LIMITED.
Miradi hii ya awamu ya kwanza inatarajia kutekelezwa kwa kipindi cha Miezi kumi na tano (15) ambapo itahusisha Ujenzi wa Barabara ya Wafipa-Kagera yenye urefu wa Km 2.434, Daraja la Mto Ruiche, Ujenzi wa barabara ya Bangwe-Burega- Ujiji yenye urefu wa Km 7.1, na Ujenzi wa mitaro ya kutiririsha maji ya Mvua katika maeneo ya Bangwe, Burega, Rutale, Mlole , Bushabani, Mji mwema, na Katonyanga yenye urefu Km 5.288.
Aidha miradi mingine inayotarajia kujengwa katika Mradi wa kuendeleza na kuboresha Miundombinu ya Miji Nchini Tanzania ( TACTICS) katika awamu ya pili na ya tatu ni pamoja na Ujenzi wa Kisasa soko la Mwanga, Ujenzi wa Kisasa wa Soko la mazao ya Uvuvi Katonga, na Ujenzi wa barabara ya Old Kasulu yenye urefu wa Km 7.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa