Na Mwandishi Wetu
Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Jana Novemba 3, 2021 ilitoa mikopo isiyokuwa na riba kiasi cha fedha za Kitanzania Million Mia moja na tano na laki tano (105,500,000/=)Kwa vikundi wajasiriamali vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Ester Alexander Mahawe ambaye alikuwa Mgeni rasmi alikabidhi mfano wa hundi la fedha hiyo kwa vikundi kumi na saba (17) ambavyo ni wanufaika vikundi kumi na tatu (13) vikiwa ni vya wanawake, vikundi viwili (02) vya vijana, na vikundi viwili (02) vya watu wenye ulemavu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Athumani Msabila alivitaka vikundi vilivyonufaika na mkopo kutumia fedha hizo kwa lengo lililokusudia ili kuleta tija na kuondoa umasikini katika jamii huku akivitaka kufanya marejesho kwa wakati
Akitaja shughuli za vikundi wanufaika wa Mkopo huo alisema ni pamoja na Utengenezaji Mikate, Sabuni, Ufumaji Shuka, Usafirishaji abiria kwa boda boda, Uendeshaji wa Mgahawa, Uchakataji wa Samaki na Dagaa , Ukamuaji Mawese na Ufugaji wa kuku wa mayai
Mikopo hiyo inatolewa kwa mjibu wa Sheria ya fedha kifungu cha 37(A) ya Serikali za Mitaa inayozitaka Halmashauri zote Nchini kutenga asilimia kumi (10%) ya makusanyo ya mapato ya Ndani
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa