Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Ester Alexander Mahawe jana Septemba 21, 2022 alifanya harambe ya kuchangia ujenzi wa Zahanati mpya katika Kata ya Kitongoni iliyopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Harambe hiyo ilifanyika ikiwahusisha Wananchi wote, Waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa idara, na vikundi vya Wajasiriamali waliohudhuria katika Mkutano huo ambapo zaidi ya mifuko ya simenti Mia mbili ( 200) zenye thamani ya Tsh 4, 800,000/= , tripu za mawe, kokoto , na mchanga vilipatikana
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya aliwapongeza Wananchi wa Kata hiyo kwa kuanzisha wazo la Ujenzi wa zahanati mpya kwa nguvu ya Wananchi huku akisema Serikali itaunga juhudi za Wananchi katika Ujenzi huo
Aidha aliwataka Wananchi hao kuzingatia Usafi wa Mji, Makazi, na maeneo ya biashara kwa lengo la kuondokana na madhara ya uchafuzi wa Mazingira kama vile Magonjwa ya mlipuko
Awali akizungumza katika Mkutano huo Meya wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Mhe. Baraka Naibuha Lupoli alsema kwa Kipindi cha Mwaka mmoja Wananchi wameanza kunufaika na miradi ya Maendeleo kutoka katika Mapato ya Ndani kama vile, Ujenzi wa Zahanati ya Machinjioni, Ujenzi wa Ofisi za Kata za Rubuga, Katubuka, Buhanda na Mwanga Kaskazini
Aidha aliwataka Wananchi wa eneo hilo kuendelea na kutoa michango yao ya fedha, vitu na ushiriki katika ujenzi wa zahanati hiyo huku akisema Manispaa hiyo itatenga vifungu vya fedha kwa lengo la kuendeleza ujenzi huo
Naye Diwani wa Kata ya Kitongoni Mhe. Himidi Omary alisema vikao vya Wananchi viliazimia kila familia itaanza kutoa kiasi cha Tsh 2000/= katika ushiriki wa ujenzi wa Zahanati hiyo
Aliendelea kusema Kata ya Kitongoni imeendelea kunufaika na Miradi ya Maendeleo ambapo Shule ya Msingi kitongoni imepokea zaidi ya Milllion 36, 000, 000/= kwa lengo la ukarabati wa Miundo mbinu na Ujenzi wa darasa moja
Miradi mingine iliyotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa Vyumba vya madarasa Matatu (3) katika Shule ya Sekondari Kitongoni kwa kiasi cha fedha Tsh 60,000,000/= huku akisema kukamilika kwa ujenzi wa bandari ya Ujiji kutawanufaisha wakazi wengi wa eneo hilo
Katika Mkutano huo Mkuu wa Wilaya aliendelea kupokea na kutatua Kero na Changamoto zinazowakabiri Wanachi katika maeneo yao ikiwemo Changamoto katika Sekta ya Maji, Ardhi, na Changamoto zitokanazo na Wanufaika wa mradi wa Tasaf
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa