Na Mwandishi Wetu
Wataalamu wa elimu Manispaa ya Kigoma/Ujiji wameanza ziara kwa Shule za Msingi tano (05) zenye changamoto ya mdondoko (kuacha/kukatiza masomo) kwa Wanafunzi.
Ziara hiyo imeanza Leo Februari 24, 2025 katika Shule ya Msingi Airport ambapo Wataalamu wa elimu kwa kushirikiana na Maafisa maendeleo ya Jamii na Ustawi wa jamii wakibainisha sababu za mdondoko wa Wanafunzi kwa kufanya vikao na Kamati ya Shule, Walimu na Wanafunzi.
Akiwa katika ziara hiyo Mthibiti ubora wa Shule Ndugu. Amri Rajab amesema lengo la zoezi hilo ni kuhakikisha kila Mwanafunzi anayeanza masomo anahitimu hadi hatua ya mwisho na Kurejesha Wanafunzi waliokatiza masomo kwa sababu mbalimbali.
Mwenyekiti wa Shule ya Msingi Airport Josephati Hamis Milenguko amesema Wanafunzi wengi wanaokatiza masomo ni wale wenye changamoto nyumbani ikiwemo kukosena kwa chakula, usimamizi wa Wazazi, na utumikishwaji wa Watoto.
Amesema ili kudhibiti mdondoko wa Wanafunzi tayari kamati ya Shule ikishirikiana na Wazazi wameweka mpango wa kuhakikisha upatikanaji wa chakula Shuleni na Ushiriki wa wazazi katika Suala la ufundishaji na ujifunzaji.
Shule nyingine zinazowakabiliwa na mdondoko ni pamoja na Shule ya Msingi Kagera, Kikunku, Kichagachui, na Kiheba.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz #shulebora
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa