Na Mwandishi Wetu
Uzinduzi huo umefanyika leo February 09, 2022 Manispaa ya Kigoma/Ujiji ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Thobias Andengenye huku akiwataka wananchi kushiriki zoezi hilo kutokana na faida zitokanazo na mfumo huo
Mkuu huyo wa Mkoa amewataka Wananchi wa Mkoa huo kuwasimamia wataalamu na viongozi watakaoshiriki katika shughuli hiyo kwa kuipa majina mitaa kutokana na Mahitaji ya wakazi wenyeji
Ameendelea kusema kufanyika kwa utambuzì na usajiri wa anwani za makazi kutasaidia kila mtu anayeishi Nchini Tanzania kuwa na anwani halisi ya makazi, utambulisho wa watu wanaoishi katika maeneo husika, usajili wa mali, biashara, na kuboreshwa kwa usajili wa vizazi na vifo
Ameendelea kutaja faida zingine zitokanazo na mfumo huo ikiwa ni pamoja na kufikisha huduma za maendeleo kwa wananchi kulingana na mahitaji yao, kupatikana kwa huduma za manunuzi kidigitali, Huduma za dharura, kama vile polisi, zimamoto na magari ya wagonjwa, zinaweza kutambua maeneo yenye dharura na kuyafikia kwa haraka, na kurahisisha zoezi la Sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika Mwezi August mwaka huu
Mkuu huyo wa Mkoa amehitimisha kwa kuwaagiza Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara na vitengo kusimamia zoezi hilo kikamilifu kutokana na faida zitokanazo na mfumo huo
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Ndugu. Rashid Mchatta awali akimkaribisha Mkuu huyo wa Mkoa amesema yupo tayari kusimamia zoezi hilo kwa Wilaya zote za Mkoa huo kwa kushirikana na Wataalamu kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa huku akisema zoezi hilo litakamilika mapema mwezi May, 2022 kama ilivyoagizo kutokana na Miji, Vijiji na Vitongoji vya Mkoa huo vingi kuwa katika mipangilio iliyobora tangu awali
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Esther Alexander Mahawe amesema usajiri wa Anwani za Makazi utaleta Mapinduzi makubwa ya maendeleo katika Wilaya na makazi ya wananchi kwa kuhakikisha huduma za Elimu, Afya na uwekezaji wa Miundombinu ya kimaendeleo inafanyika pasipo kuwa na upendeleo wowote bali kulingana na Mahitaji ya Jamii
Utambuzì wa Anwani za makazi unafanyika kwa kubandika namba za makazi, jina la barabara au Mtaa na namba ya postikodi itakayosaidia kufahamu eneo husika kidigitali, maeneo ya biashara, vitu , watu, Na Ofisi zote kusajiliwa katika mfumo huo wa kidigitali
Uzinduzi huo umehudhuriwa na Katibu Tawala wa Mkoa, viongozi wa vyama vya Siasa, Wakuu wote wa Wilaya , Meya wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri na Taasisi za Serikali na zisizo za Serikali, Waheshimiwa Madiwani, Watendaji kata na Mitaa, Wenyeviti wa Mitaa, Waandishi wa habari, wasanii, na Wananchi
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa