Na Mwandishi Wetu
Zoezi la utambuzi na uhamasishaji kwa Watoto wenye Umri wa Miaka 7-14 Wasio kuwa Shule kurudi Shuleni limeanza Leo March 05, 2023 Manispaa ya Kigoma/Ujiji Katika Kata ya Kasimbu na Kibirizi
Zoezi hilo limeanza likiongozwa na kamati ya Uhamasishaji ngazi ya Kata na Mitaa likihusisha Afisa Elimu Kata,Mwenyekiti wa Mtaa, Afisa Mtendaji Mtaa, pamoja na Wahudumu ngazi ya Jamii likilenga kuandikishwa na kuanza masomo pasipo kikwazo chochote
Zoezi hili limeanza kwa kutoa elimu kwa Wazazi na Walezi nyumba kwa nyumba na kubaini Watoto wasiopata elimu na zoezi hilo linafadhiliwa na Shirika la UNICEF
Akizungumza katika zoezi hilo Mtendaji wa Mtaa wa Kibirizi Bi. Neema Rubabwa amesema zoezi limeanza kwa ufanisi ambapo mwitikio wa Wazazi umekuwa mkubwa kutokana na awali baadhi ya Wazazi na Walezi kushindwa kugharamia mahitaji ya Watoto wao na ugumu wa maisha
Amesema Serikali kwa kushirikiana na Shirika la UNICEF watahakikisha watoto hao wanapata elimu na kupata vifaa vitakavyosaidia katika kuendelea na kuhudhuria vipindi vya masomo
Amesema zoezi hilo litaendelea kufanyika kwa kuendelea kutoa elimu kwa Wazazi, Walezi na Jamii kupitia Mikutano ya hadhara, Viongozi wa dini, Matangazo na vipindi vya radio
Zoezi hili linalenga kuwafikia Watoto ambao hawakuwahi Kusoma, utoro, kuacha Shule, na Sababu zingine ambapo wenye Umri Miaka saba (07) wataandikishwa katika Mfumo rasmi na uandikishaji wa Watoto wenye Umri wa Miaka 8-14 katika masomo ya MEMKWA ya kujenga stadi za Kusoma, Kuandika na kuhesabu na baadae kuingia katika mfumo rasmi
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa